Tegete aipa tano alliance - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday 8 February 2018

Tegete aipa tano alliance


NA RASHID HASSAN

MENEJA wa zamani wa Uwanja wa CCM Kirumba na mzazi wa mshambuliaji wa soka wa timu ya Maji Maji ya Songea, Jerrson Tegete, Mzee John Tegete, amewapongeza chuo cha kukuza vipaji (academia) ya Alliance ya mwanza kwa kupanda ligi kuu ya Vodacom.

Tegete, alisema ni pongezi na mabadiliko makubwa kwa soka la Tanzania, kwani Alliance walionesha ukomavu mkubwa wa kisoka na kuwa Akademia pekee iliyowahi kupanda ligi kuu bara hapa nchini kwa miaka ya hivi karibuni.

 wachezaji wa Timu ya Alliance
Akizungumza  na mwandishi leo , Mzee Tegete, alisema Alliance imefanikisha ndoto za mkurugenzi wao  ambaye ni Meya wa Jiji la Mwanza , James Bwire, ambapo anaamini watafanikiwa kufanya vizuri kwani wanavipaji vingi ukizingatia wengine wapo chuoni.
Alisema, anaamini Mkurugenzi wa Alliance, atafuata matakwa ya wachezaji wa ligi kuu ya Vodacom, akiwapatia wachezaji wake mikataba pamoja na kuingizwa katika ajira rasmi itakayowawezesha kumudu hali ya kiuchumi iliyopo na familia zao.

“Vijana wamepiga hatua kubwa sana, pamoja na changamoto walionesha nia ya dhati ya kutaka kuingia ligi kuu, nawaomba waendele na umoja wao na mshikamano kama walivyofanya ligi ya FDL, na hakika watafanikiwa na wataitangaza vyema mkoa wa Mwanza na na Taifa kwa ujumla”, alisema Tegete

Mbali na hayo, alimpataka Mkurugenzi wa Alliance, ktafuta wazoefu watakaoongeza morali ya kiushindani licha ya kuwepo na vipaji lukuki lakini haitawasaidia kuhimili mikiki mikiki ya ligi kuu ya Vodacom.

Pia aliitaka TFF, kugeukia Alliance wakati wa uteuzi wa timu ya Taifa na ile ya Vijana kwani anaamini chuo hicho cha vipaji kina vijana wengi wenye uwezo zaidi ya wale wanaoitwa timu ya Taifa na waliokatika ligi kuu ya Tanzania bara.


Alliance FC, ilifanikiwa kupanda ligi kuu bara ikiwa na alama 28 kwenye kundi ‘C’ nyuma ya Biashara ya mara ambao walikuwa kinara wa kundi hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot