"KMC kufanya kongamano kupongeza wachezji na maandalizi" - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday 8 February 2018

"KMC kufanya kongamano kupongeza wachezji na maandalizi"

NA YUSUPH MWAMBA

TIMU ya Soka ya Kinondoni Municipal Council (KMC), yenye maskani yake Wilaya ya Kinondoni imeandaa kongamano rasmi kwa ajili ya kuwapongeza wachezaji wake mara baada ya kufanikiwa kukata tike ya kupanda  Ligi kuu Tanzania bara msimu ujao.


Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 9 mwezi Februari, 2018 Siku ya Jumamosi   kwenye Uwanja wa Biafra kuanzia  majira ya saa 8:oo mchana.

Akizungumza na mwandishi,  Mwenyekiti wa Klabu  hiyo, Suzan Massawe,  alisema kongamano hilo ni moja ya furaha na hamasa kwa timu ya KMC kupanda ligi kuu bara kwani wataongeza morali ya ushindani na hali ya kujituma.


Alisema kongamano hilo linatarajia kuanza  mishale ya saa 6 mchana ambapo gari la matangazo litazunguka na wachezaji wa KMCkatika meneo mbali mbali ndani ya wilaya ya Kinondoni   kisha saa 8 mchana watawasili Uwanja wa Biafra tayari kwa kukamilisha kongamano hilo.

 “Huu ni utaratibu, tunawapongeza sana KMC kwani walifanya kile tulichowatuma wametubeba hatuna budi ya kuwapongeza jambo ambalo litawapa  morali ya ushindani na hali ya ushindi watakapoingia kwenye kivumbi cha ligi kuu msimu ujao”, alisema Suzan

Naye Mwenyekiti na mmiliki wa Timu ya soka ya Kinondoni FC, Saleh Alawi, aliwapongeza KMC  na kuwataka wajenge ushirikiano  imara na kujengeka kifikra katika kuelekea kwenye kinyang’anyiro cha Vodacom ambako kunaonekana kuwa na ushindani mkubwa tofauti na ligi daraja la kwanza.

KMC ambayo ilikuwa kundi C ilifanikiwa kupanda ligi kuu baada ya kujikusanyia alama 28 ikifuatiwa na Biashara ya Mara. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot