ISSRADHANS: Mahusiani na saikolojia

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot
Showing posts with label Mahusiani na saikolojia. Show all posts
Showing posts with label Mahusiani na saikolojia. Show all posts

Thursday, 26 October 2017

Sababu za wanandoa (wapenzi) wengi kuchepuka na suluhisho

October 26, 2017 0




NA  ISSA RAMADHANI,

MPENZI  msomaji wangu karibu katika safu  ya saikolojia leo, kasi ya kusalitiana kwa wapenzi(wanandoa) wengi siku hizi imekuwa ikiongezeka kila kukicha kiasi kwamba unapoingia katika uhusiano wa kimapenzi unahisi kama unaingia kwenye matatizo makubwa na hii ni sababu watu siyo waaminifu kabisa kwa wapenzi wao. Unaweza kuwa na mpenzi wako ambaye kila mnapoonana anakueleza kuwa, hawezi kukusaliti na atakuwa na wewe katika shida na raha siku zote.

wapenzi waliogombana
Utafit wa wanasaikolojia umebani uhaminifu,nin silaha kubwa kwa wanandoa (wapenzi), mbali na mila ,tamaduni katika nchi au jamiina mengine.

Lakini hivyo hivyo usishangae siku moja ukamkuta yuko na mtu mwingine. Swali la kujiuliza ni kwamba, kwa nini wanandoa(wapenzi) wanachepuka? suluhu, hiki ndicho nilichopanga kuzungumzia siku  leo. Kwa wanandoa(wapenzi)  nitaainisha baadhi ya mambo ambayo kwa uchunguzi wangu nimebaini ndiyo yanayochangia kuchepuka kwa  wanandoa (wapenzi) walio wengi kuchepuka, wawe wako kwenye ndoa au uhusiano wa kawaida.

sababu ni hizi;

TAMAA ZA KIMWILI NA PESA

Tamaa hasa ya pesa imekuwa ikiwashawishi watu kushindwa kujizuia kuwasaliti wapenzi wao. Kwa wale ambao wako kwenye ndoa wakati mwingine hasa wanawake wasipopatiwa mahitaji yao muhimu na akatokea jamaa na kumhakikishia kwamba atampatia kila anachotaka, wanakubali mara moja bila kujua kwamba wao ni wake za watu ama wapenzi wa watu na kujikuta wanajenga mazoea. Wengine wanapatiwa kila kitu na waume zao lakini sasa kinachotokea ni tamaa za kimwili tu ambazo zinawasumbua na kujikuta wanatafuta wanaume wengine huku wakidai kuwa wanatafuta ladha tofauti.

Hili si kwa wanawake tu hata wanaume pia, unaweza kumkuta ana mwanamke bomba tu mwenye kila kigezo, lakini bado anakuwa na tamaa za kutafuta kimwana mwingine nje.

TABIA ZISIZORIDHISHA 

Hapa wapo  wale  ambao wanaishi  maisha  ya  ajabu  sana, yaani wanaishi  katika(ndani) ya  ndoa  ama  wapo ndani ya uhusiano  wakielekea kwenye kuoana lakini  hawaaminiani  kabisa,  kila mtu anakuwa  na wasiwasi  juu ya mwenzake.     Afadhali  sasa  iwe kutokuaminiana  tu  lakini hapa  wapenzi  wanakuwa  hawasalitiani.
Kuna wale ambao  ni  wazi  hawatulii  katika  mahusiano yao, yaani matendo yao (tabia)  tu  yanaonesha  dhahiri kabisa  kwamba, uaminifu  ni  sifuri. Kuwa  kari bu sana  na  watu  wa  jinsia tofauti na  tabia ya kuwa na mawasiliano nao ya siri au mwanamke anapomuwekea  mumewe  vikwazo  katika  tendo la ndoa  chumbani (sex) anatarajia  akafanye wapi  na nani?  Kama  siyo kumwambia  akatafute   wengine nje?    Hii ndiyo maana  wapenzi wenye tabia wanaowanyima  unyumba waume zao hata wanaposikia  kwamba  wanasalitiwa  wanakuwa hawana  nguvu ya kuwashutumu wapenzi wao, utamshutumuje wakati wewe humtimizii  katika mambo flani? Si hivyo tu, kwa upandea wa wanaume  nao  (baadhi )wengine wamekuwa  wakiwasusa  wake zao na kukaa  siku mbili au wiki na  zaidi  bila kuonekana nyumbani  hata kama atarudi nyumbani  basi  usiku  wa manane akiwa amelewa nawew  hana  mpango kabisa wa mapenzi  na mke wake,katika mazingira hayo  unadhani  nini  kinaweza kutokea kama siyo mwanamke kutafuta mwanaume atakayempatia mapenzi? Na mume kuoa mkee mwengine .

KUWEPO  KWA MAPENZI YA KILAGHAI
(uonngo).
Tunapozungumzia  mapenzi  tunaweza  kuyagawanya  katika makundi mawili, mapenzi ya kweli na mapenzi ya uongo. Walio katika  mahusiani au mapenzi ya kweli huwezi  kuwasikia wamesalitiana. Ila wale walio katika mapenzi ya kudanganyana tabia ya kusalitiana  ni  kitu cha kawaida  kwao na hivyo  kujikuta kila siku wakifumaniana.

UDHAIFU  KWA WAPENZI 

Udhaifu  ambao umezungumziwa  hapa  ni  ule  wa  kimaumbile (big dick) ambao hata hivyo na wataalam wa masuala ya mapenzi wanaeleza  kwamba, haiwezi kuchukuliwa kama ni miongoni  mwa  sababu  ya  kumsaliti  mpenzi wako uliyempenda kwa dhati. Kwa mfano, mwanaume unakuwa ‘Functionless’ yaani jogoo hawiki (tatizo ambalo si la kujitakia)  na  mke wake  hayuko tayari kuendelea  kuwa  naye  hivyo kulazimika  kuomba  talaka.  Lakini mwanaume anakuwa  mgumu  wa  kutoa  talaka  kutokana  na jinsi anavyompenda.

Wengi  wao wanachokifanya  ni  kuendelea  kuwa  katika  ndoa huku  wakiangalia uwezekano  wa  kuanzisha au kuwa na  uhusiano  na  mtu  mwingine  wa  nje. Kwa wanawake  nao yawezekana kuwa  mwanamke hazai (tatizo  ambalo si la kujitakia pia na mwanaume anahitaji mtoto, atakachokifanya  ni kutoka(kuchepuka) nje ya ndoa yao  kwa siri lakini pia inaweza kufikia hatua mwanamke akagundua. Kwa  kifupi  ni kwamba ni c hanzo, kusalitiana kwa wanandoa  wengi  kumekuwa  kukitokea kutokana na  kuwepo  kwa mazingira fulani  ambayo  hupelekea  kuwa  baadhi yao wamekuwa  wakishindwa  kujizuia nayo  na hivyo kujikuta  wanatoka  nje  ya mahusiano yao.

SULUHISHO
Ila sasa  na lazimika kwa nguvu zote  kuwashauri  wale  walio  katika  uhusiano wa kimapenzi, namaanisha  wapenzi wa kawaida, na  wachumba  pamoja  na wanandoa, tusiwe  na tamaa za kijinga na kufikia hatua ya kuwasaliti  wapenzi wetu. Hivi unajisikiaje unapomvulia  nguo  mtu  ambaye wala hana ‘future’ na wewe? Hivi  na wewe ukifanyiwa hivyo  na  mpenzi  wako  utajisikiaje? Sasa elewa yakuwa maumivu utakayoyapata  pale  utakaposikia mpenzi wako ana uhusiano  na  Fulani  ni hayohayo atakayoyasikia mwenza (mpenzi)  wako.
NI  kuwa  muaminifu, kuridhika  na unachokipata  kwake, muoneshe mapenzi ya dhati naye  atafanya  hivyohivyo  na wote kujikuta  mnayafurahia  maisha yenu. Mfano, jadilini na kutatua matatizoyenu, kwa  pamoja  mipango  yenu ya familia, maendeleo, hali inayoleta mapenzi yenu  kuwa na furaha  na kulinda ndoa.

 
 


Read More

Chanzo na namna ya kujinasua na mapenzi ya kulelewa(Serengeti Boys)

October 26, 2017 0


Na Issah Ramadhani.

KARIBU mwanandoa mwenzangu kenye safu ya mahusiano,tubadilishane mawazo na kujuzana mambo kadhaa kama wanandoa au mchumba. Leo tutazungumzia umuhimu wa tendo la ndoa kwa wanandoa na wwatarjiwa pekee.Chanzo au sababu zinazopelekea vijana wa wenzangu wa kiume wengi kupenda  kulelewa kimapenzi na wanawake wakubwa maarufu (Mijimama) waliowazidi umri na wenyeuwezo kifedha hali hii ushawishika kwa uraisi, kuwa katika mahusianon ya kimapenzi na wengine hufunga ndoa.

jimama na mpenzi wake
Kadri siku hadi siku, wanandoa au vijana  wengi wamekuwa wakijuhusisha kuwa na mapenzi na mjimama, (Serengeti boy ) vijana wakiume  na kwa hakika tabia hii inakua kwa kasi  kubwa  mno na kuona kama jambo la kawaida, ingawa  wanasaikolojia  wanasema tabia hii ya  kupenda kitonga au kushuka katika kupata kipato na kujikimu  mahitaji yao ya kimwili,fedha na mengineyo. Ni tabia mbaya san na haifai katika jamii , mila na tamaduni zetuhazipendezi.

Hali hii imekuwa ikiwafanya hasa vijana wengi kuwa na mawazo hasi au uvivu, kwamba kulelewa na mijimama ni sawa. Bila kujali ameolewa au laha, na hivyo pia kwa mabinti wadogo kuwa na vibabu .

Swali la kujiuliza ni kwamba, kwa nini Serengeti boy hupenda kulelewa kaitika mapenzi na huwa ni wanawake wakubwa(mijimama) yenye fedha zao  waliowazidi umri mara 4 au 7  bila kujali ameolewa au ana maambukizi huwa hawa angalii hujali mapenzi na pesa.

SABABU ;

Tamaa za kutaka kuwa na maisha mazuri, Tabia hii ya baadhi ya vijna kupenda kujirahisisha au njia za mkato katika utafutaji  wa ridhiki (maisha) , hujikuta wakiangukia mikononon  mwa  mijimama wenye uwezo kifedha  na kulelewa katika maisha ,na kupata kila ancho hitaji bila kufikiria madhara au matatizo baadeye mbeleni mfano kuambukizwa na kufa  ugonjwa wa ukimwi,  migogoro kati ya familia yake na marafiki. Hapa huwa hamna mapenzi ya dhati kabisa ni kama utumwa wa mapenzi tu kwa kijana  maarufu (Serengeti Boys) wa kiume.

Uhitaji wa mtoto,Wakati mwingine hii ni sababu kwani kijana anshawishiwa na jimama kwa kila mbinu na zawadi, lengo ni kutaka mtoto na baadaye kuachana hapa ndipo kijan anapata matatizo kwa kudai mtoto wake na kutoelewana na jimam. Huenda jimama mme wake  hasababashi au haja yake ni kuzaa mtoto na Serengeti boy amtie mimba, baadaye anaachana nae. Wakati mwingine husabisha mtafaruku na kijana kupata matatizo.

Malezi mabaya ya wazazi, Ni kwa sababu Baadhi ya wazazi au walezi  tunalea watoto vibaya ,Hii nchi imekosa msingi bora wa kuwafunza watoto  shuleni kuanza kujitegemea  katika kuwafundisha shughuli ndogondogo na wazazi pia tumeiachia serikali. kama mzazi unatakiwa kumuandaa mwanao tabia ya kujifunza na  ajitegemee, awe na njia mbadala katika maisha, asifikie hatua ya kusema kwamba siwezi kufanya  hiliau lile mfano, kama akishindwa kuendelea na shule awe na ujuzi wa kazi za mikono kulima bustani,ubunifu wa kusuka mkeka, ufundi wa aina yeyote. Ili asiwe na mawazo mgando na hasi kuwa kulelewa na jimama(SUGAR MUMMY) ni dili.

kufuata mapenzi / tama za kimwili , Hapa vijan wengi hushawishiwa na mijimama(Shugar Mummy) kufanya mapenzi naye , Huenda jimama mme wake hapigi game kamili na anaamini kijan bado damu inachemka napiga game kamili na anamlizisha kimapenzi na kuwa wapenzi na kijana kupewa kila anachotaka bila kujali kuambikizwa magonjwa ya ziana na mengine ,Licha ya kukupatia  pesa na mhitaji ya kimwili na mengineyo.

Msukumo wa makundi mabaya, Kuna baadhi ya makundi katika jamii au mtani ambayo  vijana wa kiume (Serengeti Boys ) wana tabia hii ya kujishikiza kwa mijimama wenye maisha mazuri pia huwashawishi  huwashawishi na wenzao ambao hawna mpango, mawazo kuwaja ujinga  ili kujipatia na kutimiza mahitaji yao katika maisha.Tabia hii mjini inakomaa kila siku vjiana hawajishughuishi kabisa.

Ugumu wa maisha na ukata, ukosefu wa ajira na kukata tamaa ya maisha pia kukosa ubunifu na njia ya kipato kwa ufupi  umasikin  ni  sababu kubwa sana inayopelekea vijana kulelewa na mijimama kuwa wapenzi wao.
vijana  wengi tunamitizamo hasi kuwa wamama(mijimama) wanalea kutokana na kuwa ameshaanza kufanya kaz kwa miaka zaidi ya 10 na ana kipato au maisha mazuri hivo amechuma. Wakati mimi kijana(Serengeti boy) sina kitu naangaika na mtaani maisha yamezid kuwa magumu kila siku vitu vinapanda bei. Na kulalamika umasikini.

Namna ya kujinasua na mapenzi ya kulelewa (Serengeti Boys)
Suluhu , Hapa  napenda nitoe ushauri kwa kijana mwenazangu ni kujituma kwa kufanya kazi zako za utafutaji kila siku ili kufikia malengo yako. Achana na tabia ya uvivu  kuwa na ratiba nzuri katika shughuli zako ,Hii itasaidia   kuwa bize na kuepuka makundi na visahwishi , makundi mabaya na kuwakataa mijimama wakikutongoza  na kukushawishi kwa nguvu kabisa na usipende mteremko pamana na hali yako kijana , hii ni kwa wote  kiume na wakike.

Muombe mungu akupe mmke mwema , kuliko kulelewa na jimama tajiri na anakunyanyasa, kukubaka katika mapenzi. Huu ni utafiti niliufanya kwa kuwahoji vijana wa kiume na wandoa , wazazi pamoja na wahenga.Ni vema kufatuta mpenzi au mchumba  unaye mpenda kwa dhati na kuanzisha familia yako.
Read More

TIBA MARIDHAWA ZA “MAJERUHI” WA MAPENZI

October 26, 2017 0


NA ISSA RAMADJHANI,

KARIBU mwanandoa katika safu ya saikolojia, tubadilishane mawazo na kujuzana mambo kadhaa kama wanandoa na wachumba.Leo tutazungumzia tiba kwa majeruhi wa mapenzi mke au mume kusaliti ndoa husababisha kubaki na maumivu  moyoni.

Siku za hivi karibuni  wanandoa au wachumba wengi wamekuwa wakisalitiana na kuvunjika kwa ndoa nyingi,mahusiano kwa hakika tabia hii inakua kwa kasi na kuona kama jambo la kawaida, ingawa  wanasaikolojia  wanasema  uaminifu  ni silaha kubwa kwa wanandoa  (wapenzi), mbali na mila ,tamaduni katika nchi au jamii na mengine.

Imekuwa ni kwawaida sasa ndoa nyingi kuvunjika au wachumba kuachana kwa sababu kadhaa yafuata ni muhimu kuyajua na kufanyia kazi baada ya kuachana  na mpenzi wako au mchumba  kuwa  faraja ya moyo.  
wapenzi walioacha ,
Mwachie Mungu na kubali yote yaliyotokea  yapite.
Usiruhusu  mawazo yatawale kichwani mwako pindi unapoachan na mpenzi wako wa dhati na isiwe adhabu (maumivu) ,akilini mwako utajiona kama huna thamani na kuanza kujitoa kasoro kwa kujiuliza maswali mengi mfano sikumridhisha, sina mvuto na mambo mengi utafikiria.
 
Kipindi hiki unashauriwa kufunga mlango kabisa kwa ex wako , kwa kufanya maombi  kumuomba mungu upate mwingine na ikubali hali hiyo ipite  kuanza ukurasa wa maisha mengine ya furaha huku ukimuomba Mungu  sana na kusahau yote yaliopita.

Usikumbuke yaliopita mkiwa pamoja.
Tafuta kitu cha kufanya ili kukuweka bize muda wote kama mwajiliwa seikali au umejiajiri na wakati mwingine soma vitabu vya namna ya kufanya ili kupata maendeleo,Angalia tamthilia mbalimbali ,isipokuwa za mapenzi achana nazo. Ikibidi jitaidi  kutafuta marafiki wazuri wa kutoka nao  pamoja sehemu za burudanina kwa kufurahi pamoja.
 
Epuka kukumbuka ya nyuma yote ya mpenzi wako jinsi mlikuwa mnafanya na kuishi naye pamoja , labda sasa anafanyaje na mwingine, achana na hayo mawazo kabisa .
Husababisha maumivu badala yake utaumia. Hakikisha unakaa muda wa kutosha ili kutafakili akilini  mwako, kwa ajili ya kufanya mambo mengine yanayostahili maendeleo ya  maisha yako. lakini ukirudisha mawazo ya nyuma sio utaumia tu bali  hata wale wanaokuzunguka watashindwa kukusaidia.

Usianzishe mahusiano mapya kwa kukurupuka.
Kosa watu wengi wakiachika kwenye mahusiano hukimbilia kutafuta  mpenzi mpya  ndani ya muda mfupi tu ili kumuonesha ex wake kuwa na yeye anapendwa kumbe hajui hata huyo aliyempata kwa muda mfupi wahadumu nae muda mfupi na kujikuta akiachana kila uchwao.
waswahili wanasema ukiwa na furaha sana usichukue maamuzi na hata ukiwa na huzuni usifanye hivyo ni busara kutulia na muombe Mungu na mengine utafanikiwa tuu.
Nitumaini  kwa wewe ambaye bado unaugulia maumivu ya kuachwa ukizingatia haya utakuwa umepata faida wapi kwa kuanzia na kurudisha furaha na tabasam iliyokuwa imepotea.

Epuka kutuma meseji au kumfuatilia ex wako.
Jitahidi  usimtumie  meseji za kimahaba au ujumbe katita simu mfano samahani, pole, nimekosea namba kwa mpenzi wako uliye achana naye na  punguza kuongea nae ikibidi acha hadi akutafute mwenyew kwa maana kitendo cha kummtafuta utakuwa unaongeza chumvi kwenye jeraha lako mwenyewe.
Kwasasa kutokana na utandawazi uliopo ni vyema ukampa (Block) mitandaoni,namba yake ya simu ili kusiwe na mawasiliano hii itakufanya umtoe kichwani kirahisi kwani kitendo cha kumfuatilia mitandaoni kitakuumiza zaidi hebu fikiria wewe usiku mzima hujalala kutokana na maumivu ya kuachwa halafu asubuhi unaingia tuu Instagram unakutana na picha ya ex wako kaposti picha ya Mwanamke/Mwanaume mzuri halafu kaweka emoji ya vikopa kopa hapo lazima urudi kitandani uendelee kulala kuwa bize na mambo yako. 

Epuka kumsema vibaya ulieachana naye.
Mwenza wako anapoamua kuondoka na kwenda kwa mwingine usiwaambie marafiki zako kuhusu mabaya yake kwani itakufanya uonekane mtu mbaya bila wewe kujua, utaharibu mwonekano wako na tabia yako, ukimsema vibaya kuhusu yeye, pia wewe utaonekana ujitetea kuwa mkosaji, maana wakosaji bila kujiongelea mabaya yake, ndio huongea mabaya ya mpenzi wako  kwa wale ambao  hawakufanikiwa.

Epuka kusikiliza nyimbo za huzuni au kubembeleza.
Baada ya kupigwa chini au kuachana na mpenzi wako,epuka kusikiliza nyimbo za huzuni au mapenzi zenye kubembeleza hizi hasababisaha  ufikirie majanga yaliyokukuta badala yake sikiliza nyimbo za kufurahisha zenye kuchezeka na zenye kukufanya ujione wewe ni mshindi muda wote na mwenye furaha pia jichanganye na watu.

Suluhu fanya maauzi kwa  kumtafuta mpenzi baada ya kupata ushauri kwa wataalamu wa mahusaiano, wahenga(watu wazima) juu ya mapenzi ,ili kumpata mpenzi sahii kwa kuzingatia vigezo vyako ambavyo ulituma awali kumpata mpenzi mpya. Mshirikishe mungu akuongoze  katika mahusiano yako  akusimamie na chagua mwanamke mwenye kariba nzuri, mwelevu pamoja na dini madhubuti.



Read More

Post Top Ad

Your Ad Spot