TIBA MARIDHAWA ZA “MAJERUHI” WA MAPENZI - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, 26 October 2017

TIBA MARIDHAWA ZA “MAJERUHI” WA MAPENZI



NA ISSA RAMADJHANI,

KARIBU mwanandoa katika safu ya saikolojia, tubadilishane mawazo na kujuzana mambo kadhaa kama wanandoa na wachumba.Leo tutazungumzia tiba kwa majeruhi wa mapenzi mke au mume kusaliti ndoa husababisha kubaki na maumivu  moyoni.

Siku za hivi karibuni  wanandoa au wachumba wengi wamekuwa wakisalitiana na kuvunjika kwa ndoa nyingi,mahusiano kwa hakika tabia hii inakua kwa kasi na kuona kama jambo la kawaida, ingawa  wanasaikolojia  wanasema  uaminifu  ni silaha kubwa kwa wanandoa  (wapenzi), mbali na mila ,tamaduni katika nchi au jamii na mengine.

Imekuwa ni kwawaida sasa ndoa nyingi kuvunjika au wachumba kuachana kwa sababu kadhaa yafuata ni muhimu kuyajua na kufanyia kazi baada ya kuachana  na mpenzi wako au mchumba  kuwa  faraja ya moyo.  
wapenzi walioacha ,
Mwachie Mungu na kubali yote yaliyotokea  yapite.
Usiruhusu  mawazo yatawale kichwani mwako pindi unapoachan na mpenzi wako wa dhati na isiwe adhabu (maumivu) ,akilini mwako utajiona kama huna thamani na kuanza kujitoa kasoro kwa kujiuliza maswali mengi mfano sikumridhisha, sina mvuto na mambo mengi utafikiria.
 
Kipindi hiki unashauriwa kufunga mlango kabisa kwa ex wako , kwa kufanya maombi  kumuomba mungu upate mwingine na ikubali hali hiyo ipite  kuanza ukurasa wa maisha mengine ya furaha huku ukimuomba Mungu  sana na kusahau yote yaliopita.

Usikumbuke yaliopita mkiwa pamoja.
Tafuta kitu cha kufanya ili kukuweka bize muda wote kama mwajiliwa seikali au umejiajiri na wakati mwingine soma vitabu vya namna ya kufanya ili kupata maendeleo,Angalia tamthilia mbalimbali ,isipokuwa za mapenzi achana nazo. Ikibidi jitaidi  kutafuta marafiki wazuri wa kutoka nao  pamoja sehemu za burudanina kwa kufurahi pamoja.
 
Epuka kukumbuka ya nyuma yote ya mpenzi wako jinsi mlikuwa mnafanya na kuishi naye pamoja , labda sasa anafanyaje na mwingine, achana na hayo mawazo kabisa .
Husababisha maumivu badala yake utaumia. Hakikisha unakaa muda wa kutosha ili kutafakili akilini  mwako, kwa ajili ya kufanya mambo mengine yanayostahili maendeleo ya  maisha yako. lakini ukirudisha mawazo ya nyuma sio utaumia tu bali  hata wale wanaokuzunguka watashindwa kukusaidia.

Usianzishe mahusiano mapya kwa kukurupuka.
Kosa watu wengi wakiachika kwenye mahusiano hukimbilia kutafuta  mpenzi mpya  ndani ya muda mfupi tu ili kumuonesha ex wake kuwa na yeye anapendwa kumbe hajui hata huyo aliyempata kwa muda mfupi wahadumu nae muda mfupi na kujikuta akiachana kila uchwao.
waswahili wanasema ukiwa na furaha sana usichukue maamuzi na hata ukiwa na huzuni usifanye hivyo ni busara kutulia na muombe Mungu na mengine utafanikiwa tuu.
Nitumaini  kwa wewe ambaye bado unaugulia maumivu ya kuachwa ukizingatia haya utakuwa umepata faida wapi kwa kuanzia na kurudisha furaha na tabasam iliyokuwa imepotea.

Epuka kutuma meseji au kumfuatilia ex wako.
Jitahidi  usimtumie  meseji za kimahaba au ujumbe katita simu mfano samahani, pole, nimekosea namba kwa mpenzi wako uliye achana naye na  punguza kuongea nae ikibidi acha hadi akutafute mwenyew kwa maana kitendo cha kummtafuta utakuwa unaongeza chumvi kwenye jeraha lako mwenyewe.
Kwasasa kutokana na utandawazi uliopo ni vyema ukampa (Block) mitandaoni,namba yake ya simu ili kusiwe na mawasiliano hii itakufanya umtoe kichwani kirahisi kwani kitendo cha kumfuatilia mitandaoni kitakuumiza zaidi hebu fikiria wewe usiku mzima hujalala kutokana na maumivu ya kuachwa halafu asubuhi unaingia tuu Instagram unakutana na picha ya ex wako kaposti picha ya Mwanamke/Mwanaume mzuri halafu kaweka emoji ya vikopa kopa hapo lazima urudi kitandani uendelee kulala kuwa bize na mambo yako. 

Epuka kumsema vibaya ulieachana naye.
Mwenza wako anapoamua kuondoka na kwenda kwa mwingine usiwaambie marafiki zako kuhusu mabaya yake kwani itakufanya uonekane mtu mbaya bila wewe kujua, utaharibu mwonekano wako na tabia yako, ukimsema vibaya kuhusu yeye, pia wewe utaonekana ujitetea kuwa mkosaji, maana wakosaji bila kujiongelea mabaya yake, ndio huongea mabaya ya mpenzi wako  kwa wale ambao  hawakufanikiwa.

Epuka kusikiliza nyimbo za huzuni au kubembeleza.
Baada ya kupigwa chini au kuachana na mpenzi wako,epuka kusikiliza nyimbo za huzuni au mapenzi zenye kubembeleza hizi hasababisaha  ufikirie majanga yaliyokukuta badala yake sikiliza nyimbo za kufurahisha zenye kuchezeka na zenye kukufanya ujione wewe ni mshindi muda wote na mwenye furaha pia jichanganye na watu.

Suluhu fanya maauzi kwa  kumtafuta mpenzi baada ya kupata ushauri kwa wataalamu wa mahusaiano, wahenga(watu wazima) juu ya mapenzi ,ili kumpata mpenzi sahii kwa kuzingatia vigezo vyako ambavyo ulituma awali kumpata mpenzi mpya. Mshirikishe mungu akuongoze  katika mahusiano yako  akusimamie na chagua mwanamke mwenye kariba nzuri, mwelevu pamoja na dini madhubuti.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot