KOCHA Mkuu wa Klabu ya zamani wa Everton na Manchester United David Moyes amechukua ya
Slaven Bilic, ambaye alifutwa kazi siku ya Jumatatu wakati klabu hiyo
ikiwa katika nafasi ya kushushwa daraja.
Moyes amekuw bila kazi tangu mwezi Mei wakati alipojiuzulu kama mkufunzi wa Sunderland baada ya klabu hiyo kushushwa daraja.
Kocha kuu wa West Ham David Moyes |
Vile vile Mwenyekiti mwenza wa Klabu ya West Ham
David Sullivan alisema kuwa mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 54 raia
wa Uskochi ndio mtu anyefaa kurithi nafasi hiyo.
Aliongezea kufafanua kuwa Tunahitaji mtu mwenye
uzoefu ,utambuzi wa ligi ya Uingereza(EPL) na wachezaji wake na tunaamini
kwamba David anaweza kuwaimarisha wachezaji ili kuwa na kikosi imara.
Ni mtu anayeheshimika katika soka
na ataleta motisha na mawazo mapya.Alithibitisha na Everton kwamba ana
uwezo na tunadhani kwamba West Ham ni klabu ambayo itampatia fursa David
Moyes kuonyesha uwezo wake.
Mechi ya kwanza ya Moyes itakuwa dhidi ya Watford katika ligi ya Uingereza mnamo mwezi Novemba 19.
No comments:
Post a Comment