Mshambuliaji klabu ya Arsenal Olivier Giroud amezua hofu baada ya kuumia akiwa mazoezini katika timu ya taifa ya Ufaransa.
Hata hivyo Giroud amekuwa akijifua na wenzake katika eneo la Clairefontaine ili kujiandaa na mechi dhidi ya Wales, Ijumaa.
Olivier Giroud akionekana anamaumivu ya mguu pichani |
Lakini alianguka na kushikilia mguu wake chini akionyesha kuwa na maumivu, jambo ambalo linaonyesha kuzua hofu kwa Klabu ya Arsenal kuwa na majanga ya wachezji kuwa majeruhi
.
Aidha Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa Ufaransa, Didier Deschamps amesema ni tatizo dogo na halitachukua muda mrefu gerioud atakuwa amepona.
Lakini pia jambo hilo limeonekana kutowafurahisha Arsenal ambao wanaonekana wanamhitaji kwa ajili ya michuano mbalimbali ya ligi kuu Epl na michuano mengine inayowakabili mbeleni .
Mara kadhaa, kumekuwa
na mgongano kati ya klabu na timu za taifa kuhusiana na wachezaji kila upande umekuwa ukiona una haja ya kuwamiliki.
No comments:
Post a Comment