Watakaojisajili kupitia Tigo Pesa kupata asilimia 10% punguzo la bei.
Kampuni
inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali, Tigo Tanzania wakiungana na
Vision Sports wametangaza kuanza kwa usajili wa washiriki katika mbio
za Dodoma Marathon.
Mji wa Dodoma utageuzwa kuwa kitivo cha mazoezi na furaha kwa familia
nzima tarehe 12 Novemba wakati shindano hilo litakapohitimishwa.
Usajili
kwa Dar es Salaam unafanyika katika vituo maalum vya Duka la Tigo Shop
lililopo Mlimani City, Duka la Simply Elegant lililopo Dar Free Market,
Ghorofa ya Chini ya Kibo Complex eneo la Tegeta na Duka la Imalaseko
SuperMarket lilipo eneo la Posta katikati ya jiji. Kwa Dodoma, usajili
unafanyika katika eneo la Dodoma Hotel, Carnival, Cape Town Complex
iliyopo Kisasa na Duka la Tigo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
‘Wale
watakaojisajili kwa njia ya Tigo Pesa watapata punguzo la bei la
asilimia 10%. Wanaweza kufanya hivyo kwa kutuma kiasi cha shilingi
13,500/- kutoka kwenye simu zao za mkononi kwenda namba ya Tigo Pesa
0674 444 444. Hapo hapo watapokea ujumbe utakaowataarifu kujisajili na
eneo ambalo wanafaa kwenda kuchukua vielelezo vyao vya usajili,’ Meneja
wa Tigo, Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo alisema.
Kwa upande wake,Meneja wa maendeleo wa Vision Sports, Raymond Mchani kwa niaba ya Ally
Nchahaga, Mkurugenzi Mtendaji wa Vision Sports aliwashauri washiriki
kusoma vigezo na masharti ya ushiriki pamoja na taarifa nyingine muhimu
kutoka kwenye tovuti ya Dodoma Marathon na katika vituo vya usajili.
‘Pia ni muhimu kwa washiriki kuhudhuria kikao cha maelezo kuhusu
ushiriki na usalama wa washiriki kitakachofanyika kabla ya mbio kuanza
saa kumi na mbili asubuhi, pale katika Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma.
Tigo
inathamini mbio za kilometa 21 za Tigo Dodoma Half Marathon. Dodoma
Marathon pia itahusisha mbio ndefu za kilometa 42, mashindano ya
kilometa 10 pamoja na yale ya kilometa 5 yatakayohusu wanafamilia na
jamii yote kwa ujumla. Zawadi murwa zitatolewa kwa washiriki ikiwemo
vyeti vya ushiriki, medali na zawadi za fedha kwa washindi wa mbio zote.
Wanariadha mashuhuri kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki
katika mbio hizo.
“Tuna
furaha kubwa kudhamini shindano hili ambalo linahamasisha watu
kuzingatia afya bora kwa kushiriki katika michezo, na pia kuinua vipaji
katika michezo,” Henry Kinabo, Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini
alisema.
Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz
No comments:
Post a Comment