West Brom Albion yamfuta kazi mkufunzi wake - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, 20 November 2017

West Brom Albion yamfuta kazi mkufunzi wake




West Brom Albion yamfuta kazi mkufunzi wake mkuu

LONDONI,West Ham
MKUFUNZI  wa klabu ya West ham Tony Pulis  amefutwa kazi na uongozi wa klabu hiyo ikiwa pointi moja tu juu ya eneo la kushushwa daraja mbali na kutopata ushindi hata mmoja katika mechi zake 10 ilizocheza.
West Brom walicharazwa mabao 4 kwa sufuri na mabingwa watetezi wa ligi Chelsea.
Albion walishinda mechi zake tatu za kwanza msimu huu lakini wameweza kutoka sare mechi nne na kupoteza saba tangu ilipoishinda  Accrington katika kombe la Carabao 22 mwezi Agosti.
Vilevile Aliyekuwa mkufunzi wa zamani wa klabu hiyo Gary Megson ambaye alikuwa naibu wa Pulis anachukua mahala pake hadi timu hiyo itakapotoa tangazo jingine.
Mwenyekiti wa klabu hiyo John Williams aliongezea:Uamuzi kama huu hauchukuliwa kwa urahisi lakini kwa sababu ya maslahi ya klabu.
Tuko katika biashara ya kupatamatokeo mazuri lkini kutokana na matokeo mabaya ambayo yamekuwa yakishuhdiwa kufikia mwishoni mwa msimu uliopita na kufikia sasa matokeo yamekuwa mabaya.
West Brom inakutana na Tottenham ika ligi ya Uingereza katika uwanja wa Wembley siku ya Jumamosi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot