LISHE:
Juise ya viazi vitamu |
NA ODRIANI NICOLAUS
VIAZI vitamu
ni moja kati ya zao la chakula linalokuwa na kusambaa kwa kasi na upatikanaji
wake ni mrahisi karibu kila eneo hapa nchini. Ni moja kati ya vyakula na bidhaa
zenye faida lukuki kwenye afya ya binadamu.
Utafiti unaonyesha kuwa juisi
ya vitamu inapotumiwa kwa usahihi ina uwezo mkubwa wa kushambulia vimelea
vinavyosababisha ugonjwa wa saratani.
Taarifa ya mtafiti mwandamizi
wa kituo cha tiba za dawa za asilicha Paseko
Natural Health cha Tabata, Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam Dk. Othuman
Shem juisi hiyo pia ni msaada mkubwa kwa mama mjamzito katika kurekebisha mfumo
dawa na upumuaji wa mtoto tumboni kutokana na wanga uliosheheni kwenye viazi
hivyo.
Dk.Shem ambaye pia ni Katibu
Mkuu taifa wa Shirikisho la Vyama vya
Tabibu wa Asili na Mbadala anasema pia
viazi vitamu vina kiwango kikubwa cha virutubisho (vitamin A) ambayo ikiingia mwilini huweza kuifanya ngozi
kuwa nyoyororo kama mmea uliostawi kwenye mbolea ya kutosha.
“Virutubisho hivi, pia ni
muhimu sana mwilini kwani husaidia mwili kupambana na magonjwa mbalimbali kwa
kuimarisha askari (chembechembe hai
nyeupe) za damu, hivyo kuufanya mwili kuwa imara wakati wote na kutoshambuliwa na maradhi hovyo,”alisema.
Pia sukari inayopatikana kwenye
juisi ya viazi vitamu ni ya asili, ina uwezo wa kurekebisha kiwango cha sukari
kuwa cha kawaida mwilini hasa kwa wagonjwa na wetu wengine wenye dalili za
maradhi hatari ya kisukari.
Zaidi, mtaalamu huyo alisema kuwa faida nyingine ni juisi hiyo hufanya mfumo wa
uzazi wa mwanaume kufanye kazi sawasawa hasa kwa kula kuranga au kurosho wakati
huo huo juisi ya viazi vitatu ikiwa kishushio.
“ Kwa matumizi hayo mfululizo,
huweza kumfanya mtu ambaye `jogoo’ wake hawiki kufanya kazi sawasawa na
kuimarisha heshima iliyotoweka kwenye ndoa kwa matatizo hayo,”alisema.
NAMNA YA KUTUMIA:
1. Mtumiaji
anapaswa kukata vipande vidogovidogo vya viazi vitamu na kuvianika juu ya chombo safi kivulini kwa siku kadhaa
hadi vipande hivyo vikauke kwa fukuto ndani ya kivuli.
2. Sababu ya kukaushwa kivulini ni kufanya
chakula ( vipande vya viazi) kukauka kwa utaratibu na kutopoteza kiasi kingi
cha virutubisho kinachoweza kupotea ikiwa vipande hivyo vitaanikwa kwenye jua
kali.
3. Baada ya kukauka, mtumiaji , achukue
vipande hivyo na kuvisaga ili kupata
unga wake.
4. Hatua ya tatu ni mtumiaji kuchemsha maji ya moto na kutia unga
uliosagwa kwenye glasi safi.
5. Chota
kijiko kimoja cha chai (cha mezani) cha unga huo kisha changanya na maji.
Koroga hadi ipasavyo ili ichanyike vizuri. Kunywa kwa dozi ya asubuhi na jioni. Unaweza kuchanganya
asali ili kuleta ladha zaidi.
No comments:
Post a Comment