Golikipa wa Azam Razak Abarola |
NA
RASHID HASSAN
AGOLIKIPA wa klabu ya Azam Fc Razak Abarola amefikisha mechi nane(8)
bila kuruhusu kufungwa goli katika mechi 10 za ligi kuu alizoidakia timu yake hadi sasa akiwa ndioye
golikipa anaongoza kuwa na cleen sheets
nyingi kuliko magolikpa wote wa VPL baada ya mzunguko wa 10 uliomalizika
mwishoni mwa juma lililopita.
Razak akiwa anacheza ligi kuu
Tanzania bara kwa mara ya kwanza huku akimkalisha benchi golikipa wa muda mrefu
wa timu hiyo Mwadini Ali amefanikiwa kumzidi golikipa wa Peter Manyika Jr wa
Singida United mwenye cleen sheet saba baada ya kucheza mechi 10.
Ambapo Manyika Jr alimfikia Razak kwa kucheza mechi saba bila kuruhusu goli (Manyika
alipocheza mechi yake ya 10 vs Lipuli, wakati huo Razak alikuwa amecheza mechi
9) lakini baada ya Razak kucheza mechi ya 10 na kutoruhusu goli amemzidi
Manyika kwa cleen sheet moja zaidi baada ya magolikipa hao kucheza mechi 10
kila mmoja.
Mechi nane (8) ambazo amecheza
Razak amecheza bila kuruhusu goli
Katika clean cheets nane za Razak
nne kati ya hizo Azam alishinda huku mechi mbili zikimalizika kwa suluhu (0-0).
·
Ndanda 0-1 Azam
·
Azam 0-0 Simba
·
Azam 1-0 Kagera Sugar
·
Azam 1-0 Lipuli
·
Mbao 0-0 Azam
·
Aza 1-0 Mbeya City
·
Azam 1-0 Ruvu Shooting
·
Njombe Mji 0-1 Azam
Magolikipa wengine wanaofutia
kucheza mechi nyingi bila kufungwa
·
Peter Manyika Jr (7)
·
Aishi Manula (6)
·
Youthe Rostand (6)
·
Benedict Tinoco (6)
No comments:
Post a Comment