Na
Mwandishi wetu
Dk. Peter Landless |
WATAALAMU
wa afya wameishauri jamii kuzijua hesabu za kukokoto kiwango cha unene ili afya
zao na tatizo la unene uliopitiliza kulingana takwimu za Shirika la Afya Duniani
(WHO) kuonyesha kuwa watu milioni 2.8 hufariki dunia kila mwaka kwa unene.
Wataalamu hao Dk.
Peter Landless wa kitivo cha tiba cha chuo kikuu cha Maryland nchini Marekani
anasema tatizo la unene ulipitiliza zimezidi kuwaathiri watu wengi kutokana na
kutozingatia kanuni za ulaji na vyakula.
Dk. Landless ambaye
pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya
Kimataifa ya Kuzuia ulevi na dawa ya kulevya (ICPA) chuoni hapo alisema tatizo
hilo limekithiri katka nchi tajiri na zanazoendelea ambapo
ikiwamo Tanzania.
“Unaweza kukokotoa kiwango cha unene ambao huelezwa
kama usio wa mlundikano mkubwa au uliokithiri wa shahamu unaoweza kudhuru afya,
kwa kutafuta kiashirio cha uzito wa mwili wako (Body Mass Index BMI)” alisema.
Naye Dk. Mark Finley pia wa chuoni hapo anashauri
kuwa ili kufanya hesabu hiyo ni lazima kugawa uzito wako katika paundi kwa
kipeo cha pili cha urefu wa mtu husika katika inchi kisha kuzidisha kwa 703.BMI
yako 25 au zaidi una uzito mkubwa…na kama ni 30 au zaidi, utambue kwamba una
ugonjwa wa kunenepa kupita kiasi,alisema.
Anasema fomyula katika vipimo vya metriki ni (uzito
katika kilo)/(urefu katika mita x uzito katika mita) akitolea mfano uzito wako
kama ni kilo 60 na urefu wa mita 1.70 BMI=60/(1.7X1.7)=20.8 (upo katika
kategoria ya kawaida).
Matatizo mengi ya kiafya hutokana na uzito
uliokithiri ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo, shinikizo
la damu na baadhi ya saratani.
“Hata hivyo moja kati ya magonjwa yaliyoenea zaidi
ni kisukari ambacho tutazingatia hapa…zaidi ya theluthi ya watu bilioni moja ulimwenguni
wana kisukari takribani mtu mmoja katika kila 20 duniani nchi zenye uwezekano
mkubwa wa ugonjwa wa kisukari.
Kufikia mwaka 2030 nchi zitakazoongoza kwa ugonjwa
huo duniani ni China, India na Marekan. Unene uliokithiri huelezwa kama mtu
mwenye uzito uliozidi uzito wake wa kawaida kulingana na urefu wake kwa
asilimia 20 ya watu wenye kisukari namba ya 2 wana uzito uliokithiri. Maradhi
haya mawili yanahusiana na kiasi kwamba wataalamu wengi wa afya huyachukulia
kama ugonjwa mmoja, ambao wanauita diabesity (kisukari kitokanacho na umeme).
Kiwango cha kisukari kimeongezeka kwa watu wa
kawaida katika miaka ya karibuni, kama matukio ya unene uliokithiri ambao ni chanzo
cha kwanza cha mgagonjwa ya kisukari yanavyoongezeka. Kila mwaka kiasi cha watu
milioni 3.4 hufa kutokana na matatizo yanayoletwa na kisukari na kwamba
tathimini inaonesha kuwa kisukari kitakuwa ugonjwa wa 7 duniani kwa kusababisha
vifo ifikapo mwaka 2030.
No comments:
Post a Comment