Abortion.
NA ODRIAN NICHOLAUS,
KUTOA mimba ni nini? Hii ni hali ya mwanamke kwa hiari yake
mwenyewe kuharibu mimba iliyoingia ndani ya kizazi chake.
Kutokana
kuongezeka kwa idadi ya mahusiano duniani na kutotumia njia za uzazi wa mpango
kwa watu wengi walioko kwenye mahusiano, wasichana wengi kwa sasa wanatoa mimba.
Siyo Tanzania pekee ni duani ani ni
janga.
UTAFITI
nilioufanya mwenyewe nimegundua kuwa
zaidi ya asilimia tisini ya wasichana wanaokua kwenye mahusiano na wanaume
zaidi ya mwaka mmoja kabla ya ndoa hutoa mimba na asilimia tano tu ya wote wanaamua kuzaa. Sio ajabu kusikia mtu ameolewa
akiwa ametoa mimba nne mpaka tano. Sasa unajiuliza bado kuna mtu humo au mfu?
Hata
hivyo hao wanaozaa pia hujikuta wamebeba mimba zingine wakati watoto wao wakiwa
wadogo na kulazimika kuzitoa. Najua watu wengi wanatoa mimba kukwepa aibu,
kutokua tayari kisaikolojia na kadhalika lakini ni bora kutumia njia za uzazi
wa mpango kama condomu kuzuia mimba na kama kondomu huiwezi basi tumia njia
zingine kama sindano na vijiti kwasababu wengi wenu mkishalewa pombe au kondomu
isipokuepo ndio basi tena.
Hebu tuyaangalie madhara ya kutoa mimba kama ifuatavyo…
Uwezekano mkubwa wa kufa:
Utafiti
uliofanywa na madaktari wa finland mwaka 1997 umegundua kwamba wanawake
wanaotoa mimba wanauwezekano wa kufa mara nne zaidi kuliko ambao hawatoi mimba.
Vifo hivyo vimekua vikisababishwa na kujiua wenyewe kutokana na kujuta kwa
maamuzi yao na madhara ya mda mrefu ya kimwili yatokanayo na kutoa mimba. Vifo
ndani ya wiki moja baada ya kutoa mimba hutokana na kuvuja damu sana, madhara
ya dawa za usingizi, mabonge ya damu kwenye mishipa ya damu na mimba iliyotunga
nje ya uzazi. Utafiti pia uliongeza kutoa mimba moja uwezekano wa kufa unakua
45%, mimba mbili 114%, mimba tatu 192%.
Ugumba kwa wanawake wengi:
Miaka
hii ya karibuni wanawake wengi ambao wanalia kutopata watoto wana historia za
kutoa mimba miaka iliyopita, na wengi wao nilionana nao wanajuta sana kwa
maamuzi yao. Hii inatokana na madhara makubwa waliyoyapata kwenye mfuko wa
uzazi baada ya mimba kutoka.
Mimba kutunga nje ya kizazi:
Mfuko
wa uzazi una utando maalumu amaboa hufanya mimba iliyotungwa kwenye mirija
iitwayo fallopian kuwezesha yai kushuka hadi kwenye mifuko ya uzazi. Lakini
utoaji wa mimba huambatana na magonjwa ya mirija hiyo na kupoteza utando huo na
kusababisha mimba kukulia huko.matibabu ya tatizo hili ni kukata mrija husika
tu hivyo kuongeza hatari ya ugumba..
Kuzaa
watoto wasio na akili nzuri:
Utoaji
wa mimba kuharibu mlango wa mfuko uzazi kushindwa kushika vizuri na matokeo
yake mwanamke huyu hujikuta akizaa kabla ya mda husika akibeba mimba nyingine.
Lakini pia watoto hawa wanaozaliwa kabla ya muda maalumu na viungo
ambavyo havijakomaa hupata shida ya ubongo na kua wagonjwa wa akili maisha yao
yote.
kansa ya
mlango wa uzazi
Wanawake
wanaotoa mimba wana hatari kubwa ya kupata kansa ya mlango wa uzazi kuliko
wengine ambao hawajatoa mimba. Hii ni kwasababu ya kusumbuliwa kwa mlango huo
kwa dawa za kutoa mimba, vifaa vya kutoa mimba na mabadiliko ya ghafla ya
homoni za uzazi.
Kuathirika kisaikolojia;
Hakuna
mwanamke ambaye hatakaa ajutie maamuzi yake ya kutoa mimba siku za usoni hata
kama hakupata madhara yeyote hii itamfanya aishi kama ana deni Fulani maisha
yake yote na itakua inamuumiza usiku na mchana. Zingine ni kukosa hamu ya kula,
kusikia sauti ya mtoto anayelia wakati hayupo, kua na hasira sana…
Ushauri.
kumbuka
kila mwaka wanawake 70000 wanakufa kwa kutoa mimba...maumivu ya kukosa mtoto ni
makali sana kuliko aibu ya kuzaa nje ya ndoa. Hawa wanaozaa sasa hivi unawaona
malaya ipo siku utawakumbuka utakapo ambiwa na daktari kwamba labda itokee
miujiza ndo utazaa.Kama hutaki mimba tumia njia za uzazi wa mpango kwani
kuendelea kutoa mimba kutakupa adhabu ya kukosa mtoto ambayo adhabu hiyo
utaitumikia maisha yako yote.

No comments:
Post a Comment