WAFUNGWA walioko katika magereza mbalimbali katika mkoa wa Mara,
watajifunza kilimo cha zao la pamba wakikwa gerezani hili wamalizapo kifungo
chao wawe waelimishaji kwa wananchwalioko katika maeneo yao kuhusu kilimo
hicho, jambo ambalo litasaidia viwanda vya zao hilo kupata mali ghafi ya
kutosha.
Hayo yalielezwa jana
na mkuu wa mkoa wa Mara Adamu Malima, wakati akizindua shamba darasa la zao la
pamba la mkoa wa huo lilikoko katika enao la Kisangwa wilayani Bunda.
Malima alisema
kuwakilimo cha zao la pamba, lazima kindelezwe ili kuinua uchumi wa mkoa huo na
nchi kwa ujumla na hivyo hata wafungwa walioko gerezani lazima wafundishwe
kilimo cha zao hilo ili wamalizapo vifungo vyao wakawe mabalozi wa kilimo cha
zao la pamba katika jamii inayowazunguka.
Aidha, alisisitiza
wananchi kulima zao hilo la pamba ili viwanda vyetu viweze kuapata mali ghafi
ya kutosha na kwamba pia wananchiwalime mazao mbalimbali ya chakula ili
kukabiliana na upungufu wa chakula.
Hata hivyo Malima
alisema kuwa gereza la Mkoa wa Mara, tayari limekwishatenga jumla ya ekari 300
kwa ajili ya kiimo cha zao hilo wakishirikiana na halmashauri ya wilaya ya
Butiama.
“Hili shamba tunataka
liwela mfano kweli kweli….JKT pia wamekubali kuingia kwenye kilimo hiki cha
pamba, lakinipiawakulima wadogowadogo na na nyinyi pia muendelee kulima kilimo
cha zao hili. Lakini pia taasisi mbalimbali nazo zilime zao hili, tunataka mkoa
wa Mara uwe namba moja katika kilimo cha zao la pamba” alisema Malima.
Baadhi ya wananchi
walipongeza mpango na hatua hiyo ya serikali mkoani hapa kwa kuhamasisha kilimo
cha zao la pamba, ikiwa ni pamoja na kuwepo mashamba darasa, ambapo sasa
watalima kilimo chenye tija zaidi hali itakayowasaidiakujiinua kiuchumi.
“Mimi kama mkulima kwa
kweli nimefurahishwa sana na mpango huu wa serikali yetu, zamani tulikuwa
tunalima kiholelahleholela tu kwa kutupa mbegu sasa elimuhii itatusaidia sana”
alisema Nestory Madulum mkulima wa kijiji cha Kisangwa.
Akitambulisha mpango
huo wa shamba darasa afisa kilimo wa mkoa wa Mara, Denis Nyakisinda alisema
kuwa huu mpango wa shamba darasa ameuleta mkuu wa mkoa huo, Adamu Malima, ili
zao hio liwe kubwa na la kibiashara katika Mkoa huo.
Mkuu wa mkoa wa Mara,
Adamu Malima alisema iwapo wakulima mkoani humo wakizingatia kiimo hicho
watazalisha tani laki moja za zao la pamba, ambapo kwa kufuata kilimo chenye
tija kila ekari moja ina uwezo wa kuzalisha kilo 800 hadi 1000, ambapo kwa sasa
wakulima wanazalisha kilo 300 mpaka 400 kwa kila ekari moja.

No comments:
Post a Comment