 |
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki
Ulisubisya akimjulia hali mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji mkubwa wa mgongo,
anayetoa ufafanuzi wa namna upasuaji huo ulivyofanyika ni Dkt. Nicephorus
Rutabansibwa (Daktari bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mgongo). Kushoto ni
Mganga mkuu wa Serikali Profesa Muhamed Kambi.
|
NA MWANDISHI WETU.
TAASISI ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo,
Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) imeokoa zaidi ya shilingi Bilioni 5 ambazo
zingetumika kusafirisha wagonjwa nje ya nchi kufuata matibabu baada ya MOI
kuanzisha huduma za kibingwa ambazo awali zilikua hazipatikani hapa nchini.
Hayo yamebainishwa katika ziara ya Katibu Mkuu
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na watoto Dkt. Mpoki
Ulisubisya alipotembelea MOI na kukagua hali ya utoaji wa huduma, mazingira ,
miundombinu na kuwajulia hali wagonjwa pamoja na kukutana na menejimenti.
Akizungumza na menejimenti ya MOI, Dkt.
Ulisubisya amepongeza kazi nzuri na kubwa inayofanywa ambayo imepelekea
watanzania kupata huduma bora za kibingwa ambazo wangepaswa kuzifuata nje ya
nchi.
 |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya akikagua mashine mojawapo katika benki ya damu ya MOI.
“Mnafanya
kazi nzuri sana, jambo ambalo linatupa faraja kubwa sisi viongozi wenu, naomba muongeze ubunifu zaidi, hamtakiwi
kuifikiria MOI kwenye ukanda huu wa Afrika pekee bali duniani, hii ni changamoto
kwetu sote kuifikisha hapo ”alisisistiza Dkt. Ulisubisya
Aidha, Dkt Ulisubisya amesema MOI imepunguza rufaa za kwenda nje
ya nchi kwa asilimia 95% na asilimia 5% iliyobaki MOI inaweza kuimaliza kabisa
na kusiwepo mgonjwa wa kwenda nje ya nchi.
Pia, amewaelekeza viongozi wa MOI kushirikiana na Wizara ya Afya
kutafuta namna ya kufuta rufaa kwa kutoa mapendekezo na ushauri
utakaosaidia kutatuliwa kwa changamoto hiyo.
 |
Mtaalamu
wa Maabara Bwana Mbuta Jackson akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya
,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya kuhusu namna
benki mpya ya damu inavyofanya kazi kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa damu
salama.
Azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ni kuhakikisha huduma zote za Afya zinapatikana hapa nchini na vyema sote tukamuunga mkono” amebainisha Dkt. Ulisubisya.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Muhamed Kambi amepongeza uongozi wa MOI kwa kuwa na maono ya mbali ya kuifanya MOI kuwa Taasisi bora barani Afrika na Duniani.
“Nimefurahi kwamba MOI mna maono ya mbali, mnafikiria kuitoa Taasisi hii hapa ilipo na kuifikisha sehemu ya juu zaidi, dira yenu ni kuwa Taasisi bora Afrika kufikia 2022 fanyeni kazi kwa bidii kufikia lengo hilo.” amesema Prof Muhamad Kambi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na
Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya ( katikati ) akiwa katika picha ya pamoja na
menejimenti ya MOI. (Picha na:
MOI)
Awali
akiwasilisha taarifa ya Utendaji, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt Respicious
Boniface amesema toka kuanzishwa kwa Taasisi hiyo imefanikiwa kuanzisha huduma
za kibingwa za Upasuaji wa Nyonga, Magoti, Ubongo, Mgongo, Vibiongo, Usingizi
ambazo zimesaidia kupunguza rufaa za nje ya nchi.
“Baada ya kuanzisha huduma hizi za Kibingwa tumefanikiwa kuokoa
shilingi Bilioni 5 ambazo zingetumika kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi,
tumepunguza rufaa kwa asilimia kubwa naomba nikuhakikishie hata hizi asilimia
5% zilizobaki tutashirikiana na Serikali na naamini zitakwisha kabisa.” amesema
Dkt. Respicious Boniface.
|
|
No comments:
Post a Comment