![]() |
| Shule kongwe ya Sekondari Ndanda |
NA MWANDISHI WETU.
WAHITIMU wa Shule kongwe ya Sekondari Ndanda iliyopo Masasi mkoani
Mtwara, kupitia umoja wao (UWAHISSENDA) wanakusudia kuanzisha kampuni
itakayotoa mikopo midogomidogo kwa lengo la kujiimarisha kiuchumi.

Hatua hiyo imekuja miaka miwili baada ya wahitimu hao kuanzisha
kundi
la mtandao wa kijamii la Whatsaap lenye zaidi ya wanaumoja 250, na
hivyo hivi karibuni kuazimia pamoja na kuimarisha umoja wao, wafikirie
pia kuinuana kiuchumi.

Akizungumza baada ya kikao cha wanaumoja hao hivi karibuni, Kaimu
Mwenyekiti wa UWAHISSENDA, Yohana Kasawala alisema dhamira yao itaanza
kutekelezwa mapema mwakani baada ya kuwa tayari wameshapata mtaji
kutokana na michango ya wanachama.

Alisema, pamoja na kukopeshana huku riba ikitumika kutunisha mfuko
wa
umoja, wanakusudia kutanua wigo wa mikopo hata kwa wasio wanaumoja wa
UWAHISSENDA.

Aidha, mipango hiyo ya kuinuana kiuchumi inakwenda sambamba na
mpango
wa uzinduzi wa umoja huo uliopangwa kufanyika shuleni Ndanda mapema
mwakani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 90 tangu kuanzishwa
kwa shule hiyo.

“Daima umoja ni nguvu, utengano ni dhaifu, nasi tumeona ni vyema
tukatumia mshikamano huu kama fursa ya kujiimarisha kiuchumi. Tuna
ndoto nyingi, lakini kwa kuanzia tunakuja na hili la kampuni ya mikopo
midogomidogo yaani Microfince company…

“Wataalamu wetu wa uchumi ndani ya umoja ambao wametapakaa katika
taasisi za fedha nchini wametupatia mchanganuo wenye kutia matumaini
kwamba tutaweza, na kama mambo yatakwenda hivyo, siku za usoni
tunaweza kufikiria hata kuanzisha benki…Ni suala la muda tu,” alisema
Kasawala na kuongeza kuwa, umoja una Katiba, umesajiliwa kisheria na
kufuata taratibu nyingine za nchi.

Ndanda, shule iliyoanzishwa mwaka 1928, ni miongoni mwa shule kongwe
zilizotoa wasomi wengi waliobahatika kushika nyadhifa mbalimbali
katika nchi, miongoni mwao akiwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.
Pia wamo Hawa Ghasia, mmoja wa mawaziri waandamizi katika Serikali
ya
Awamu ya Nne chini ya Utawala wa Rais Jakaya Kikwete. Subira Mgalu,
Naibu Waziri wa Nishati katika Serikali ya Rais, Dk John Magufuli pia
ni matunda ya sekondari ya Ndanda.

No comments:
Post a Comment