Obrey Chirwa amekabidhiwa kitita cha kiasi fedha tasilimu TSh milioni moja. |
NA ISSA RAMADHANI.
MSHAMBULIAJI wa Kimataifa kutoka Klabu ya Yanga, Obrey Chirwa amekabidhiwa kitita cha kiasi fedha tasilimu
TSh milioni moja.
Aidha Chirwa amekabidhiwa fedha hizo za mchezaji
bora wa Oktoba wa Ligi Kuu Bara baada ya kuwashinda wachezaji Ibrahimu Ajib na
Erasto Nyoni wa Simba.
Hata hivyo Chirwa
aliisaidia Yanga kupata alama saba kwenye
michezo mitatu huku akifunga jumla ya magoli matatu na kutoa pasi
mbili za magoli.
No comments:
Post a Comment