KENYA,Nairobi

Wafuasi wa upinzani wamekuwa wakikabiliana na polisi
mara kwa mara tangu Agost.
Muungano wa upinzani umetangaza kwamba
hautambui sherehe hiyo na haumtambui Bw Kenyatta kama rais aliyechaguliwa na
wananchi.
Kiongozi mkuu wa upinzani Raila Odinga
amepanga kuandaa mkutano mkubwa wa kuwakumbuka watu waliofariki wakati wa
makabiliano kati ya wafuasi wa upinzani na polisi.
Odinga na muungano wake wa National Super
Alliance (Nasa) wamesisitiza kwamba mkutano huo utafanyika katika uwanja wa
Jacarada, Nairobi, takriban kilomita kumi hivi kutoka uwanja wa Kasarani ambapo
sherehe ya kuapishwa kwa Bw Kenyatta itakuwa inaendelea.
Bw Kenyatta alipata asilimia 98 ya kura katika
uchaguzi wa marudio, ushindi ambao uliidhinishwa na Mahakama ya Juu
iliyofutilia mbali kesi mbili zilizokuwa zimewasilishwa na wanaharakati wawili
na mbunge wa zamani kupinga uchaguzi huo.
Serikali imesema viongozi 20 wa mataifa
mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo ya kuapishwa kwa Bw Kenyatta,
akiwemo kiongozi wan chi jirani ya Tanzania Dkt John Magufuli.
Mwezi uliopita, ripoti ya Tume ya Taifa ya
Haki za Binadamu ilisema watu 37 waliuawa tangu kutokea kwa uchaguzi wa tarehe
8 Agosti.
Tume hiyo iliwatuhumu polisi kwa kutumia
nguvu kupita kiasi wakikabiliana na wafuasi wa upinzani.
Idara za usalama nchini Kenya zimekanusha
tuhuma hizo.
No comments:
Post a Comment