Fiesta yawaunganisha Yamoto Band wafanya Show kali. - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, 27 November 2017

Fiesta yawaunganisha Yamoto Band wafanya Show kali.

NA ISSA  RAMADHANI.

TAMASHA la fiesta 2017 limemalizika  Jumamosi hii  lililofanyia Leaders Club jijini Dra es salaam ,tulishuhudia wasanii wa Kundi la Yamoto Band wakiungana pamoja kama zamani na kufanya show ya pamoja na kuleta msisimko mkubwa kwa mashabiki waliojitokeza ukumbini hapo.
Image result for FIESTA DAR 2017 YAMOTO BAND

Ambapo asilimia mia (100%)  ni kutoka hapa Tanzania pekee wasanii waliopafomu jukwaani . kwa ubunifu mwingi katika show na mashabiki wengi wa burudani walijitokeza kushuudia show hiyo.

Wasanii wa kundi hilo kwa sasa kila mmoja anafanya kazi kivyake huku Aslay pamoja na Beka Flavour wakionekana kufanya vizuri kutokana na vibao vyao walivyovitoa hivi karibuni kupendwa zaidi na mashabiki.

Akiongea na mashabiki waliojitokeza kwenye tamasha hilo, Aslay amewataka mashabiki kujipanga kwa ajili ya kibao kipya cha kundi hilo.

“Asanteni sana mashabiki kwa upendo wetu kuna kitu kipya tunawaandalia,” alisema Aslay baada ya kumaliza show yao hiyo.

Katika show hiyo Maromboso ndiye msanii pekee wa kundi hilo aliyekosekana huku baadhi ya wadau wakidai muimbaji huyo anajiunga na WCB ndio maana ameshindwa kuonekana tena akiwa pamoja na kundi.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot