LONDON,EnglandMshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku huenda akapigwa marufuku mechi tatu ikiwa ni pamoja na debi ya Manchester - iwapo FA wataamua kumuadhibu mchezaji huyo wa miaka kwa 24 kwa kile kinachoonekana kuwa kama kumpiga teke beki wa Brighton Gaetan Bong.
Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji amesifiwa sana na meneja wa Manchester United Jose Mourinho, licha ya kutofunga bao lolote katika mechi tisa kati ya 10 alizochezea klabu hiyo karibuni. (Guardian
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema winga wa Wales Gareth Bale, 28, hatauzwa wakati wa dirisha ndogo la kuhama wachezaji Januari. (Daily Star)
Mabingwa wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya wanapanga kuwasilisha ofa ya £80m kutaka kumchukua mshambuliaji Mfaransa anayechezea Manchester United Anthony Martial, 21, majira yajayo ya joto. (Daily Mirror)
Arsenal nao wako tayari kutathmini ofa zenye uzito za kutaka kumchukua mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez, 28, na viungo wa kati Mesut Ozil, 29, wa Ujerumani na Jack Wilshere, 25, wa England mwezi Januari. (Daily Express)
No comments:
Post a Comment