WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani S. Jafo
(Mb) amesema jumla ya watumishi wa Sekta ya Afya wapatao 2058 wamekwisha
pangiwa vituo vya kazi kuanzia leo 06/11/2017 na taarifa zote
zinapatikana kwenye mtandao wa Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali(Tamisemi) Selemani Jafo |
“Taarifa ya watumishi 2058
imekamilika na itarushwa kwenye mtandao wa OR TAMISEMI leo tarehe
6/11/2017 jioni, hivyo Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa
Halmashauri zote nchini wanatakiwa kujiandaa kuwapokea watumishi hao
ikiwemo kuwapatia stahiki zao”
Amewataka Wakurugenzi wa Mamlaka
za Serikali za Mitaa na Waajiri kuhakikisha wanachukua taarifa za
watumishi walioripoti na kuwaingiza kwenye Mfumo wa Mishahara na
kuwapangia katika maeneo ambayo ya uhitaji mkubwa ili kuboresha huduma
za afya nchini.
Pia ameekeza watumishi wanaopangiwa vituo, kuripoti katika vituo vyao vya kazi ndani ya siku 14 tangu tangazo hili kutolewa.
Aidha, Waajiri wote watoe taarifa
juu ya kuripoti kwa watumishio haa wapya na vituo walivyopangiwa siku 14
baada ya kuripoti kwao.
Taarifa za Watumishi hao na Vituo
vyao vya kazi, inapatikana katika Mtandao wa Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) wa www.tamisemi.go.tz
No comments:
Post a Comment