KOCHA mpya wa
Everton, Sam Allardyce amesema kwamba wachezaji wamepoteza hali ya kujiamini na
ameiagiza klabu kusajili mbadala wa Romelu Lukaku.
Mwalimu huyo mwenye wa miaka 63 ,leo
amethibitishwa kuwa kocha mpya wa Everton
na mwanahisa mkuu wa klabu, Farhad Moshiri amemtaja kama kiongozi wa nguvu' na
amemtabiria ataifikisha timu panapohitajika.'
Lakini kuelekea utambulisho rasmi, Allardyce ameandika kwenye safu ya Paddy
Power na kutoa maoni yake juu ya kufanya
vibaya kwa timu hiyo msimu huu wa ligi kuu Epl
The Toffees wanashika nafasi ya 17 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England pointi
mbili tu kutoka nafasi za kuteremka daraja, licha ya kutumia Pauni Milioni 140
kufanya usajili mzuri kwa lengo la kumaliza ndani ya sita bora.
Allardyce amekiri klabu ipo katika nafasi mbaya kwa sasa na amesema jukumu lake
la kwanza litakuwa ni kurejesha hali ya wachezaji kujiamini.
Allardyce amerejea kutoka mapumzikoni
leo na kukutana na Moshiri kusaini mkataba wa kufundisha Everton.
Ambapo mkufunzi huyo atakuwa anapokea mshahara Pauni Milioni 6 kwa mwaka katika
miezi 18 ya mkataba wake na ataanza rasmi kazi jumamosi katika mchezo wa Ligi
Kuu ya England dhidi ya Huddersfield Town Uwanja wa Goodison Park.
Lakini leo atakwenda kushuhudia mchezo dhidi ya West Ham.na kubaini wapi aongeze kungu na mfumo pamoja na mbinu za ushindani.
No comments:
Post a Comment