Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akihamasisha ulimaji wa zao la Pamba kwa
wakulima wa Wilaya ya Urambo Mkoani humo wakati wa ziara yake ya kikazi
kuhamishisha shughuli za maendeleo.
Hata hivyo Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa mkutano wake na wanavijiji wa Wilaya ya Urambo waliojitokeza na kumweleza kero mbalimbali ikiwemo uhaba wa kuwa mbegu za pamba kufuatia wengi wao kuonesha nia ya kulima zao hilo.
Alisema kuwa baada wakulima wengi kupatiwa elimu ya uhamasishaji juu ya kilimo cha kisasa cha zao hilo ikiwemo uzingatiaji wa sheria na kanuni za ulimaji wa pamba kumekuwepo na mwitikio mkubwa wa wanakijiji kutaka kulima zao hilo.
Baadhi
ya wakazi wa Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa mkoa
huo Aggrey Mwanri alipofanya ziara katika wilaya hiyo kuhamasisha shughuli za
maendeleo ikiwe kilimo cha zao la Pamba.
Mwanri alisema kuwa si vema
kuwakatisha tamaa wakulima hao kwa sababu ya ukosefu wa mbegu na dawa za kuua
wadudu, hivyo ni vema Bodi ikalishughulikia suala hilo kwa haraka zaidi.
“Bodi nawaombeni sana msije
mkanifanya nionekane mwongo kwa kuwaambia wakulima kuwa mbegu zitapatikana na
kisha zisifike …hawataniamini tena” alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Alisema kuwa Mkoa wa Tabora ndio
uliochaguliwa kuwa mzalishaji wa mbegu za pamba na kitalu cha taifa kwa
ajili ya maeneo mengine nchini, hivyo mbegu pekee inayohitajika kupandwa ni
UKM08 katika maeneo yote.
Mwanri alitoa wito kwa Bodi hiyo
kuhakikisha kuwa upungufu wa mbegu hizo unaondolewa na zinawafikia wakulima
mapema kwa sababu mvua zimeshaanza kunyesha na kuna baadhi ya maeneo mkoani
humo zinakuwa ngumu kupitika katika kipindi hicho.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya
Urambo Angelina Kwingwa alisema kuwa katika msimu ujao wa kilimo makisio yao
ilikuwa kupokea tani 31,020 lakini hadi sasa wamepokea tani 19,398 na
kusambazwa katika vijiji 56 kati ya 57 vilivyokisiwa kulima zao hilo.
Alisema kulingana na hamasa
iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa katika maeneo mbalimbali wakulima wengi
wamehamasika ambapo wameongezeka kutoka 4,268 hadi kufikia 4,689.
Kwingwa alisema kuwa hali hiyo
inawafanya wanahitaji nyongeza ya tani 36 za mbegu ili waweze kukamilisha kwa
wakulima wote.
Naye Meneja wa Bodi ya Pamba
Tanzania, Kanda ya Magharibi Jones Bwahama alisema kuwa hakuna mkulima ambaye
hatashindwa kulima zao hilo kwa sababu ya kukosa mbegu za pamba.
No comments:
Post a Comment