CHUO KIKUU
Huria pekee kimepewa ruhusa ya kuendelea kutoa kozi ya Foundation iliyokuwa
imesitishwa na serikali kwa wanafunzi ambao wamekosa vigezo vya kujiunga na
elimu ya Chuo Kikuu baada ya mtaala wake kuboreshwa na kupitishwa na Wizara ya
Elimu.
Ruhusa hiyo imetolewa na Waziri Mkuu
wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa leo akiwa mkoani Singida yanapofanyika
Mahafali ya chuo hicho.
Ikumbukwe kuwa Mwaka 2016 Naibu
Waziri wa Elimu, Mhandisi Stella Manyanya alitoa katazo hilo na kusema
utaratibu wa kozi ya Foundation umefanywa na vyuo vyenyewe hivyo
serikali haiwezi kuukubali mfumo wa elimu hiyo na kwamba kama mtu anasoma
kozi ya Foundation apewe cheti na kama atahitaji kujiendeleza asafishe
cheti au asome mfumo ambao utamfikisha katika shahada.
Mbali na hayo katika Mahafali hayo
ambayo Waziri Mkuu ndiye Mgeni rasmi atamtunuuku mkewe Bi Mery Shahada ya
Uzamiri ya Elimu.
"Wakati najiandaa kuja kwenye
sherehe mwenzangu naye kumbe anajiandaa, nashukuru amemaliza sasa mambo
nahisi yataenda vizuri maana wakati mambo ya masomo yalipokuwa busy hata
tulikuwa hatuonani...Leo pia naona familia yangu nayo itakuwa
inasherehekea" Majaliwa
Pamoja na hayo Waziri Mkuu
amejipigia debe sherehe ya mahafali yajayo yakafanyike mkoani Lindi pia kwani
wamejiandaa vyema
No comments:
Post a Comment