Mchezaji wa Klabu ya Azam Fc ,WAaziri jinior |
NA
ISSA RAMADHANI.
MSHAMBULIAJI wa klabu ya soka
ya Azam FC nchni Tanzania,Wazir
Junior amefiwa na mama yake mzazi usiku wa
kuamkia leo nyumbani
kwao
Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zimethibitisha msiba huo ambapo tayari mchezaji
huyo amepewa ruhusa ya kwenda nyumbani kwa ajili ya kushiriki msiba huo wa mama yake.
Aidha Klabu ya Azam FC imepokea kwa masikito makubwa msiba huo mzito wa mama yake Wazir hivyo
imeungana na familia nzima kwenye
kipindi hiki kigumu.
Hata hivyo Wazir alikuwa amesafiri na timu kuelekea Njombe kwa ajili ya
mchezo wa ligi wikiendi hii dhidi ya Njombe Mji, lakini tayari ameenza
safari ya kurejea Dar es salaam asubuhi hii ambapo ataunganisha hadi Lushoto
Tanga.
Uongozi wa Azam FC kwa niaba ya mashabiki na
klabu kwa ujumla, umetoa salamu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki
pamoja na familia ya Junior.
No comments:
Post a Comment