Kubeza viwanda ni mtazamo finyu - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, 17 November 2017

Kubeza viwanda ni mtazamo finyu




 Mh Jenista  Joakim Mhagama akizungumza mjini Dodoma.


 NA MWANDISHI WETU.

WAZIRI  wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu  Jenista  Joakim Mhagama  amesema kuwa mapinduzi yoyote ya viwanda huanza  na  viwanda vidogo  hivyo  watu  wasibeze  dhana  ya  viwanda  nchini .

Ambapo Mh. Mhagama  ameyasema hayo mjini Dodoma wakati akichangia mada kwenye kongamano la pili la kitaaluma la kuwasilisha matokeo ya tafiti juu ya mchango wa viwanda katika ukuaji wa uchumi endelevu.

“Maendeleo ya viwanda Tanzania kama ilivyo nchi nyingine yanatokana na kuwekeza nguvu katika viwanda vidogo, vya kati na hatimaye viwanda vikubwa na hakuna  mapinduzi  yoyote  katika  nchi  kubwa  yaliyoanza  na  viwanda vikubwa”. Alisema.

Aidha waziri Mhagama  ameongeza  kuwa wapo watu  wanaobeza  viwanda vidogo  na  dhana  nzima  ya  viwanda  nchini  ambapo  amesema  huo ni mtazamo finyu na umepitwa  na wakati.

Waziri amewaomba wananchi kuunga mkono sera ya viwanda kwa kuanza na viwanda vidogo kisha viwanda vya kati na hatimaye lengo la kuwa na viwanda vikubwa litatimia kupitia kuanza na viwanda vidogo.

----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

No comments:

Post Top Ad

Your Ad Spot