“Jezi ya Di Maria Iilikuwa dili Manchester United pekee” - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, 17 November 2017

“Jezi ya Di Maria Iilikuwa dili Manchester United pekee”





LONDON,Manchester.

KATI ya usajili ambao Luis Van Gaal aliufanya  ukawa gumzo dunia nzima ulikuwa ni usajili wa Angel Di Maria kutoka Klabu ya Real Madrid  baada ya msimu mmoja tu waliamua kuachana naye  akaenda  PSG.

Wakati Di Maria akiondoka kwenda PSG hakuna bosi wa United alihangaika kumbembeleza abaki katika timu yao na walionekana walikuwa tayari kumuacha mchezaji huyo aondoke ndani ya muda mfupi.

Sasa Imebainikwa kwamba Manchester United walikuwa wakihitaji zaidi mauzo ya jezi ya Di Maria kuliko walivyokuwa wakihitaji uwepo wake katika timu hiyo na hilo lilimkera Muargentina huyo.

Aidha Msemaji wa mchezaji huyo amethibitisha kwamba United hawakumhitaji Di Maria ,ili  kushinda makombe na walikuwa wakiambiana kwamba wakimnunua atawasaidia sana katika mauzo ya jezi.

Debora Gomes amesema “Di Maria hakuwa na furaha ndani ya United na mabosi hawakuwa na habari naye huku akisema baada ya Fergie kuondoka sasa United imekuwa klabu ambayo haiwazii kuhusu soka tena bali jinsi ya kuingiza pesa tu.

Mnamo  Mwaka 2014   United walitoa kiasi cha £59m  kwa  Real Madrid  ili kumnunua na inasemekana hadi anaondoka United walishauza jezi za Di Maria ambazo ziliwaingizia zaidi ya £75m.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot