NA MWANDISHI WETU.
Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Taasisi ya Kimataifa ya
Kiislamu ya Misaada (IIRO) ya Saud Arabia wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa
kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization) kwa
kutumia mtambo wa Cathlab katika kambi ya matibabu ya moyo inayoendelea JKCI.
Jumla ya wagonjwa 40 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ya siku
tano.
Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge na mwenzake wa Taasisi ya Kimataifa
ya Kiislamu ya Misaada (IIRO) ya nchini Saud Arabia, Ali Al Masoud wakimfanyia
mgonjwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono
(Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab katika kambi ya matibabu ya
moyo inayoendelea kwenye Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 40 wanatarajiwa
kufanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ya siku tano.
Zoezi la kumfanyia mgonjwa upasuaji
wa kuzibua mishipa ya moyo kupitia mshipa wa damu wa mkono (Catheterization)
kwa kutumia mtambo wa Cathlab likiendelea.
No comments:
Post a Comment