Rais Joseph Kabila
KONGO,Kinshasa
MAASKOFU wa Kanisa Katoliki nchini
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wamemtaka Rais Joseph Kabila kujitokeza
hadharani na kutangaza kuwa hatagombea urais kwa muhula wa tatu.
Kauli hiyo ya Maaskofu imekuja baada ya
mkutano wao kuthamini hali ya kisiasa nchini humo huku kukiwa na na shinikizo
kutoka Jumuiya ya Kimataifa, kwa serikali ya DRC kuhakikisha uchaguzi huo
unafanyika kama ilivyopangwa.
Hata hivyo hayo yanajiri wakati ambapo
serikali ya DRC imepiga marufuku maandamano yaliyopangwa wiki hii kushinikiza
kujiuzulu kwa Rais Joseph Kabila.
Muelekeo kuhusu Uchaguzi Mkuu nchini DRC
umepangwa kufanyika nchini humo mwezi Disemba mwakani 2018 .
wakati huo upinzani wa nchi hiyo
umekuwa ukidai kuwa Kabila, anapanga kuwania tena kinyume cha katiba,
madai ambayo Rais huyo bado hajajibu.
No comments:
Post a Comment