mwamuzi Elly Sassi kutoka tanzania
NA ISSA RAMADHANI,
WAAAMUZI wawili wa
soka kutoka hapa nchin Tannzania wameteuliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika
Mashariki na Kati (CECAFA) kwa ajili
kuchezesha michuano ya Kombe la CECAFA
Challenge itakayofanyika nchini Kenya.
CECAFA imewataja mwamuzi wa kati Elly Sasii na mshika
kibendera Soud Lila, kutoka Dar es Salaam kuwa sehemu ya waamuzi wa michuano ya
CECAFA 2017.Waandaji wa michano hiyo ni nchi ya Kenya .
Mbali na waamuzi hao, CECAFA pia imewateua kocha Sunday Kayuni ambaye amewahi kuwa
Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF na
Mjumbe Mteule wa Kamati ya Utendaji ya TFF
Ahmed Iddi Mgoyi kuwa wajumbe wa Kamati ya Maandalizi.
Waamuzi hao wawili na wajumbe wawili
wanatarajiwa kusafiri kwenda nchini Kenya Novemba 30 mwaka huu, tayari kwa
kushiriki taratibu nzima za maandalizi hayo ambapo michuano itaanza Desemba 3 hadi 17 mwaka huu.
Ambapo Timu ya taifa ya Tanzania Bara
Kilimanajaro Stars na ile ya Tanzania Visiwani Zanzibar Heroes zipo kwenye
maandalizi ya michuano hiyo. Timu hizo zimepangwa kundi moja sambamba na timu
za Libya na Rwanda.
No comments:
Post a Comment