Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Jumaa Aweso (wa kwanza kulia) akikagua sehemu ya mtambo wa kutibu wa kutibu na
kusafisha maji wa Matogoro, pamoja na Meneja Ufundi wa Mamlaka ya Maji na Usafi
wa Mazingira mjini Songea (SOUWASA), Mhandisi John Kapinga.
NA MWANDISHI WETU,RUVUMA
NAIBU waziri wa Maji na
Umwagiliaji, Jumaa Aweso amesisitiza kuwa wizara yake haitakuwa kikwazo cha
utekelezaji wa ahadi ya Rais, Dkt. John Magufuli ya kuwapatia wananchi majisafi
na salama, bali itasimimamia utekelezaji wa miradi hiyo ipasavyo ili ikamilike
kwa wakati na kuleta tija.
Aweso alizungumza hayo
katika ziara yake ya kikazi aliyoianza katika mkoa wa Ruvuma, ambapo anakagua
utekelezaji wa miradi ya maji katika wilaya zote mkoani humo.
Mtambo
wa kutibu na kusafisha maji wa Matogoro, Songea Mjini, mkoani Ruvuma
‘‘Niwahakikishieni
wizara haitakuwa kikwazo katika utekelezaji wa miradi ya maji nchini, zaidi ya
kuhakikisha miradi yote tunayoitekeleza inaleta tija na kumaliza kero ya maji
kwa wananchi kulingana na maagizo ya Rais. Hivyo, lazima fedha zifike kwa
wakati na zitumike kwa usahihi ili miradi yote ikamilike kwa wakati kulingana
na mikataba,’’ alisema Naibu Waziri.
‘‘Ni jukumu langu
kusimamia hilo na ninawaagiza watendaji wote wasimamie miradi yote hatua kwa hatua
na watoe taarifa sahihi za maendeleo yake, ili sisi viongozi tujue changamoto
na kutoa msukumo katika kufanikisha miradi hiyo itakayokuwa na tija na
thamani halisi ya fedha zinazotumika,’’alisisitiza Aweso.
Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji ametoa pongezi kwa SOUWASA kwa usimamizi mzuri wa miradi na hatua
inazozichukua kwa nia ya kumaliza kero ya maji katika maeneo ya mji huo kama
Midizini na Misufini ambayo yalikuwa na kero kubwa, lakini kwa sasa wananchi
kukiri kupata huduma hiyo.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso
akishuka baada ya kukagua tanki la mradi wa Mtendewawa, wilayani Songea Mjini,
mkoa wa Ruvuma.
Katika ziara hiyo
ameanza kwa kutembelea Wilaya ya Songea, ambapo ametembelea Mamlaka ya Majisafi
na Usafi wa Mazingira mjini Songea (SOUWASA) na kuweza kuzungumza na
menejimenti yake, pamoja na watumishi.
Aidha, alitembelea
miradi mbalimbali inayotekelezwa katika wilaya hiyo ikiwemo eneo la mradi wa
Bwawa la Luhira, mtambo wa kutibu na kusafishia maji wa Matogoro, mradi wa
upanuzi wa mtandao wa majisafi Songea.
Huduma ya maji kwa mji
wa Songea kwa sasa ni asilimia 79, ambapo lita milioni 10.6 zinazalishwa kwa
siku na mahitaji yakiwa ni lita milioni 14 kwa siku kwa wakazi wa mji huo.
Upanuzi wa mradi wa maji wa Songea mjini unaondelea hivi sasa unategemea
kuongeza upatikanaji wa maji kwa asilimia 90 kwa mji wa Songea.
No comments:
Post a Comment