Kocha mwenye lesenin A kufundisha Tanzania - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, 17 November 2017

Kocha mwenye lesenin A kufundisha Tanzania






NA ISSA RAMADHANI.



SHIRIKISHO  la soka nchini TFF limemtangaza mchezaji wa zamani wa Tanzania Ammy Ninje kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania bara maarufu kama Kilimanjaro Stars.

Akizungmza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Afisa habari wa shirikisho hilo Alfred  Lucas amesema kocha huyo mwenye leseni A ya ukocha kutoka  shirikisho la soka barani Ulaya( UEFA)  ataiongoza Kilimnjaro  Stars kwenye  michuano ya  CECAFA Challenge  mwaka huu.

Katika hatua nyingine Alfred amesema kocha Ammy  kesho anatarajia kutangaza majina ya wachezaji wa kikosi hicho watakaokwenda nchini Kenya kuwakilisha Tanzania bara kwenye michuano hiyo.

Aidha Ammy Conrad Ninje ambaye  mchezaji wa zamani wa Tanzania ambaye amecheza soka na kujifunza ukocha katika nchi za Ulaya na Amerika. Hatua kubwa ambayo amewahi kufikia ni kuwa kwenye benchi la ukocha la timu ya Hull City ya nchini England.

Hata hivyo Michuano ya CECAFA Senior Challenge inatarajiwa kuanza Desemba 3 hadi 17 mwaka huu.

Timu ya Kilimanjaro Stars imepangwa kundi A na nchi za Kenya, Libya, Rwanda na Zanzibar katika michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot