Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi
Duce, Profesa Rwekaza Mukandala
NA MWANDISHI WETU.
CHUO Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (Duce) kinakabiliwa na deni la Sh700 milioni,
lililotokana na mkopo uliotolewa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB)
ikiwa ni gharama za kusomesha wanataaluma.
Aidha Rais wa chuo hicho, Profesa William Anangisye amesema hayo kwenye mahafali ya kumi ya Duce jijini Dar es Salaam.
Alisema ili kukabiliana na madeni kutoka bodi hiyo, chuo kimeanzisha utaratibu wa kuwachuja wanataaluma wanaoomba kusomeshwa na bodi.
“Tumeanzisha uhusiano na vyuo rafiki nje ya nchi ili vitusaidie kusomesha wanataaluma hawa,” alisema.
Vile vile Anangisye amefafanua kuwa huu ni wakati wa wanataaluma kutafuta ufadhili kutoka taasisi nyingine za kimataifa zinazotoa ufadhili ili wasomeshwe.
Alisema wanatumia fedha nyingi kuwalipa wahadhiri wa muda chuoni hasa katika masomo ya Fizikia, Hisabati, na Infomatiki.

No comments:
Post a Comment