Na Peter Mwamkamba
MENO ni kiungo muhimu kwa maisha ya kia
binadamu, hata hivyo kuna aina nyingi ya utunzaji wa kinywa chako ili kisitoe
harufu mbaya pamoja na kuyafanya kuwa imara zaidi.
Leo Daktari kutoka nchini India
anayeshughulikia tiba ya meno, Meet Ramatri, anafafanua njia
bora za utunzaji bora wa kinywa na meno yako.
Anasema osha meno yako mara mbili kila
siku. Tumia uzi ili kusafisha maeneo ambayo hayafikiwi na mswaki ili kuondoa uchafu kwenye maeneo yanayounganisha jino moja
na lingine.
Aidha, anasema futa kinywa chako kabisa
baada ya kula chakula chochote. Hii itafuta au kuondoa mabaki ya chakula
ambacho kinapatikana kwenye sehemu za meno na pia hupunguza uchafu unaotokana
na rangi ya chakula kwenye meno.
Anashauri kutumia mswaki wenye dawa ya
meno ili kuondoa vipande vilivyopo kwenye meno na uchafu wa chakula ambao umekusanywa ndani ya meno.
Pia anasema punguza ulaji wa chakula kinachoweza kufanya kinywa chako kuwa safi kwa muda mdogo, kupunguza ulaji wa chakula laini na kichafu a kwamba vyakula vitamu (vyenye sukari) huwa vinakaa kwenye meno kwa muda mrefu hasa juu ya meno na kuanzisha kuoza kwa jino.
Anashauri kuiwekea utaratibu wa
kusafisha fizi mara kwa mara, kumia chakula cha afya kilicho na wingi wa
protini, vitamini na kalsiamu.
Ansema matumizi ya dawa ya meno ya
fluorid husaidia kudhibiti uharibifu wa jino
kwa watoto wadogo, hivyo ni vizuri kutumia
mswaki wenye dawa ya meno wenye nyuzi zenye uwezo wa kupenye sehemu za wazi au
mashimo ya kudumu na fika kwa mtaalam wa meno mara moja kila baada ya miezi minne au sita kwa uchunguzi wa kawaida.
EPUKA YAFUATAYO
Dokta Ramatri anashauri ili kulinda meno yako na
kuyafanya kuwa imara epuka sigara kwani husababisha meno yako kuoza.
Aidha anasema epuka matumizi ya
vinywaji vya kusindika ambavyo vinaweza kufuta tabaka la meno na epuka kula
chakula kigumu sana ambacho kinaweza kusababisha kuvunjika kwa meno.
Anashauri kujiwekea tabia kama kusaga
au kuunganisha meno yako wakati wa usiku ambayo inajulikana kama bruxism ambayo
huzuia kuenea kwenye uso wa meno. Hii inazuia kutoboka au kufanya meno yabadilike katika
hali isiyo ya kawaida, kuvaa meno na kuhakikisha yanadumu kwa muda mrefu pamoja
na viungo vya taya.
IDW (India Dental World)

No comments:
Post a Comment