RC atoa agizo la kufanya biashara - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, 26 October 2017

RC atoa agizo la kufanya biashara



Na Mwandishi wetu.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameziagiza Halmashauri zote zilizopo Mkoani kwake kuhakikisha wanakuwa na magulio rasmi ya kuuzia mahindi ili, wakulima na wafanyabiashara waweze kufuata utaratibu . 

Aidha  Mh. Zelote amesema kuwa kwa kufanya hivyo kutakuwa na usimamizi thabiti na taratibu za uingizwaji wa bidhaa kutoka katika nchi za jirani utafuatwa pamoja na kuwa mamlaka husika kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria zilizopo ikiwa ni pamoja na halmashauri kupata mapato na nchi kwa ujumla.


Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen  pichani
Kauli hiyo ameitoa baada ya kufanya ziara ya ghafla katika Kijiji cha Safu, kilichopo mpakani mwa Tanzania na Zambia na kujionea malori yenye shehena za mahindi yakiingizwa kiholela kutoka katika nchi ya Zambia bila ya kuwepo kwa mamlaka 
husika zinazosimamia uingizwaji wa bidhaa kutoka katika nchi za jirani.

"Ni mategemeo yangu kuwa wakurugenzi wataanzisha vituo ili wakulima waweze kupeleka mazao yao hapo na kuweza kuyauza na ndipo nao halmashauri waweze kukusanya ushuru unaotakiwa, lakini hizi biashara zinazofanywa kupitia njia za panya, nasema si kitu cha kuachiwa, hivyo basi nisingependa kuona malori yanaruhusiwa kwenda maeneo ambayo siyo mipaka rasmi kuchukua mizigo na kuingiza nchini," Amesema.

Na kuongeza kuwa hakuna tatizo kufanya biashara na nchi za jirani isipokuwa biashara hizo zifanywe kihalali kwa kufuata sheria zilizowekwa na chi husika .
Akifafanua  Mh. Zelote Alisema kuwa Mkoa wa Rukwa una mahindi ya kutosha na wafanyabiashara wa mikoa mingine wafike kununua na sio kuvuka mipaka kwa njia za panya kufanya biashara hiyo.

Kwa upande wao wafanyabiashara waliohojiwa na Mh. Zelote katika ziara yake hiyo walidai kuwa mahindi yanayotoka Zambia bei yake ni nafuu zaidi kuliko ya Tanzania lakini pia wakulima wa Tanzania huficha mahindi yao wakisubiri kupanda kwa bei jambo ambalo ni hasara kwa wafanyabiashara wanaotoka nje ya Mkoa wa Rukwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot