Harry Kane kuikosa Manchester United ? - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, 26 October 2017

Harry Kane kuikosa Manchester United ?


LONDON,Manchester.
Kocha wa klabu ya Tottenham Hospurs Mauricio Pochettino amekataa kusema iwapo Harry Kane ni majeruhi au alimpumzisha tu kwaajili ya mchezo wa jumamosi dhidi ya Manchester United kwenye uwanja wa Old Traford. 
Harry Kane kushoto  na kocha
 Mauricio Pochettino

Kane mwenye miaka 24 ,jana alikuwa nje ya kikosi cha Tottenham kilichokubali kichapo cha mabao 3-2 dhidi ya West Ham kwenye kombe la Ligi maarufu EFL, ambapo Tottenham walikuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani  Wembley.

Aidha Alipoulizwa na wahandishi wa habari kuhusu sababu za Kane kuwa nje.Pochetinho aligoma kueleza sababu huku akionesha kuwa na mashaka endapo nyota huyo atakuwepo kwenye mchezo wa Manchester United Jumamosi hii.

Sio lazima awe anaumwa, kuna muda tunalazimika kuwapumzisha wachezaji kwahiyo suala la kucheza mechi ijayo tutaona nafikiri sio muda sahihi kueleza hilo”, alisema Pochettino.

Tottenham na United zinalingana pointi zikiwa na 20 kila mmoja baada ya mechi tisa, nyumba ya vinara Manchester City wenye alama 25 lakini vijana wa Jose Mourinho ni wa pili kwa tofauti ya mabao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot