Sababu wanaume kufa mapema kuliko wanawake katika ndoa - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, 26 October 2017

Sababu wanaume kufa mapema kuliko wanawake katika ndoa



NA ISSA RAMADHANI.

KARIBU msomaji wangu katika safu hii ya saikolojia. Ni siku nyingine tena kwa neema yake Mungu amejaalia tubadilishane mawazo na kufahamishana mambo kadhaa  muhimu katika maisha yetu ya kila siku.
wapenzi wakifurahi pamoja.
Leo tutazungumzia sababu za wanaume kufa mapema kuliko wanawake katika ndoa au uchumba.
Utakubaliana na mimi kwamba wanaume wengi walioko kwenye ndoa wanakufa mapema na kuwaacha wake au wachumba wao wakiwa katika hali ya huzuni na majonzi.
Ni mipango ya Mungu binadamu kufa lakini wakati mwingine sisi binadamu wenyewe hujisababishai au kusababishiwa kifo bila kujua au kwa kujua.  
  
Kisaikolojia baadhi ya wanaume walioko kwenye ndoa hufa mapema na kuwaacha wake au wapenzi na familia. Hapa nitaeleza baadhi ya chanzo cha wanaume kufa mapema kuliko wnawake katika ndoa.
MSONGO WA MAWAZO
Wanaume ndio waathirika wakubwa wa tatizo la msongo wa mawazo (stress),  ingawa kwa nje wanajitahidi kuonyesha kuwa mambo yako shwari wakati wanatafunwa ndani kwa ndani.
Utafiti mdogo unaonyesha wanaume hospitalini wanaokufa kwa presha ya kupanda au ya kushuka, kiharusi, moyo kusimama, kupasuka kwa mishipa ya damu, matatizo  ya mifupa au maimivu ya kichwa chanzo kikubwa ni msongo wa mawazo.

USIRI
Wanaume wengi ni wasiri, ni wagumu kueleza au kuweka wazi yanayowasibu na kubakia kuugulia moyoni.
Wengi hawapendi kuwashirikishi watu wengine matatizo yaliyopo katika ndoa zao hata pale yanapokuwa sugu na kuwafanya waishi bila ya amani huku wakiwa na msongo wa mawazo usioisha.
Wako tayari wafe na tai shingoni wakijifanya hawaumii au hawana tatizo.
Baadhi ya wanaume wakiwa  na tofauti kwenye ndoa zao zao wakaitwa sehemu kuyaongea ili kupata ufumbuzi pale zinapokuwa nje ya uwezo wao, huwawapati, anaweza kukwambia mambo yetu tutasuluhisha wenyewe wakati ndani kwa ndani yanamla na hatimaye kummaliza kiafya na hata kusababisha kifo.

KUTOJALI AFYA
Ni rahisi sana mwanaume akajisikia vibaya asiende hospitalini kwa wakati kuangalia afya yake tofauti na mwanamke.
Hata pale anapohimizwa kwenda anaweza kukwepa au kuwa mbishi au hata kudanganya ameshakwenda au ameshakunywa dawa kumbe mwongo.
Tabia hii husabaisha  ugonjwa kuwa mkubwa na husababisha kifo kwa uzembe wa kujali afya.

KUTOSAMEHE
Kusamehe sio tu kwa faida ya anayesamehewa bali pia kwa afya yako unayesamehe. Mzigo unaoutua kutokana na kusamehe huondoa maumivu moyoni na kumaliza msongo wa mawazo.
Baadhi ya wanaume ni wagumu sana kusamehe. Wako tayari wayabebe moyoni  matatizo kwa miaka hali amabyo inawamaliza bila wao kujua.

TABIA HATARISHI
Wanaume wengi kwenye ndoa wanaoongoza kushiriki tabia hatarishi kama vile ulevi, anasa, ngono holela na tabia hizi  huwaweka karibu zaidi na jeneza kuliko wake zao wanaowaacha nyumbani.
 Kibaya zaidi hata wanapopata maambukizi ya magonjwa, watoto wa nje ya ndoa huwadanganya hawawaambii ukweli wenza wao na kusababisha matatizo makubwa zaidi katika familia.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot