Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, nchini James Kilaba |
Aidha, imezitaka kampuni zinazorusha
matangazo ya luninga kufuata sheria na kanuni za usajili zinazowataka kurusha
bure matangazo ya chaneli za ndani.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James
Kilaba, amesema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye, alipofanya ziara
katika ofisi hizo.
Kilaba alisema kuhama kutoka
analojia kwenda digitali ilikuwa ni kazi kubwa ambayo lazima ingeleta
changamoto ambazo wanaendelea kuzifanyia kazi.
Alisema kampuni hizo zimekuwa
zikikata matangazo ya chaneli za ndani pindi muda wa kifurushi alicholipia
mteja kumalizika licha ya mkataba walioingia na TCRA kuelekeza kuwa huduma hizo
zitatolewa bure kwa wananchi.
Alisema anatambua kuwapo mvutano
kati ya kampuni za urushaji matangazo na watoa huduma wa kituo kuwa nani
anapaswa kulipia gharama hizo na ni kiasi gani na kwamba wanalitafutia ufumbuzi
suala hilo ili wananchi wapate chaneli hizo bure.
Chaneli zinazotakiwa kupatikana bure
ni ITV, TBC, Star TV, Chanel Ten, Clouds TV na TV Tumaini.Naye Naibu Waziri
huyo, aliwataka TCRA kusimamia kanuni na sheria hizo ili wananchi wapate huduma
hizo bila malipo yoyote.
Aidha, Nditiye, aliitaka TCRA
kufunga vibanda vyote vya kusajili laini za simu bila kufuata sheria.Alisema
kumekuwapo na idadi ya vibanda na watu wakipita mitaani bila kuwa na
vitambulisho na kusajili laini bila kuzingatia kanuni na taratibu za usajili
hali ambayo inapelekea baadhi yao kuzitumia kufanya uhalifu.
“Tunataka kila mtu anayetumia laini
awe anafahamika. Na taratibu zitumike kama ilivyopangwa kuwa vitambulisho
vinavyotakiwa kutumika ni vya kupigia kura au cha uraia. Napendekeza ikiwezekana
usajili uwe unafanyika kwenye ofisi za watoa huduma badala ya watu kusajili
ovyo mitaani,” alisema.
No comments:
Post a Comment