CHADEMA wamlipua Mtulia, wadai njaa zake zimempeleka CCM - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, 6 December 2017

CHADEMA wamlipua Mtulia, wadai njaa zake zimempeleka CCM


MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilaya ya Kinondoni, Waziri Mhunzi, kwa niaba ya chama hicho, ametoa tamko kufuatia kujivua uanachama wa CUF na nyadhifa zote kisha kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia.

Akizungumza na waandishi wa habari, Ndugu Mhunzi, amewaomba wananchi watulie na wasikate tamaa, wasidhani kwamba kuondoka kwa Mtulia, basi UKAWA Umekufa au umeyumba au CHADEMA Watakata tamaa, hilo jambo halipo.
Image result for (CHADEMA), Wilaya ya Kinondoni, Waziri Mhunzi.
“Mtulia ni msaliti na dhambi ya usaliti atakuja kuiona hapahapa duniani, kabla hajaondoka, hajafa na kwenda kaburini, kabla hajawa maiti ataona dhambi ya usaliti.
“Siku ambayo matokeo yanatangazwa, tunapigania atangazwe watu watatu waligongwa na gari pale Biafra, wawili walipona na mmoja akafariki, na walikuwa katika harakati za kupigania kutangazwa kwa Mtulia” amesema Mhunzi. 

Aidha Mwenyekiti huyo wa CHADEMA Kiondoni, ameongeza kuwa licha ya kusalitiwa na Mtulia, pia Usaliti mwingine umefanywa na Chama cha Mapinduzi (CCM), ambacho kinawasaliti Wananchi wake kwa kutumia, Rasilimali na kodi za Wananchi, kuwarubuni viongozi wa upinzani waingie CCM.

“Kumuunga mkono Magufuli siyo kwenda CCM, Bali ni kuwatumikia Wananchi,” alisema Mhunzi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot