“Google Kuajiri watu wa kuondoa Video zilizokuwa na maadili” - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

tanzania

Post Top Ad

Wednesday, 6 December 2017

“Google Kuajiri watu wa kuondoa Video zilizokuwa na maadili”

Your Ad Spot

utjh7rdme7f0obonu3ct

New York, Marekani.


KAMPUNI ya Google inayomiliki mtandao wa kurusha video wa Youtube imeanza kuajiri watu wa kupitia video na kuondoa zilizo kinyume na maadili.

Vile vile Mtandao huo pia umeanzisha kanuni kali zitakazosaidia kuondokana na kadhia ya video zinazokinzana na maadili.

Mkakati uliop hadi mwakani, kampuni hiyo imepanga kuajiri watu 10,000. Mkurugenzi wa Youtube, Susan Wojcicki amesema wataajiri watu wengi zaidi Desemba na Januari,2018.

Amesema wanalazimika kufanya hivyo kwa sababu katika kipindi cha miezi sita wameshuhudia video zaidi ya 2 milioni  zilizokuwa zikichochea uhalifu na nyingine za ugaidi.

"Tutafuatilia maoni yanayotolewa na watazamaji pia, tutayaondoa iwapo yatabainika yana nia ovu ya kushambulia au kuchochea uhalifu,” amesema Susan.

Mtandao wa Youtube uliingia matatani hivi karibuni baada ya kudaiwa kuwapo video za udhalilishaji watoto. Kampuni nyingi kubwa duniani zilijiondoa kutangaza katika mtandao huo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad