LONDON,England.
KAMPUNI ya Facebook imezindua mtandao mpya wa kijamii wa kutumiwa
na watoto wa chini ya miaka 13.
Mtandao huo ambao umeundwa kwa njia
sawa na mtandao wa Messenger ambao huwawezesha wanaoutumia kuwasiliana kwa
kutumiana ujumbe utakuwa ukiitwa Messenger Kids.
Facebook kwa kawaida imekuwa
hairuhusu watoto wa chini ya miaka 13 kutumia mtandao wake mkuu wa Facebook.
Lakini taarifa zinasema wapo wengi
ambao huhadaa kuhusu umri wao na kwamba inakadiriwa watoto zaidi ya 20 milioni
wa chini ya miaka 13 wanatumia mtandao wa Facebook.
Messenger Kids inatarajiwa kuwapa
watoto ufahamu kuhusu nembo ya Facebook na hivyo kuongeza uwezekano wao kusalia
kwenye mtandao huo. Facebook wamechukua hatua hiyo huku wakiendelea kupata
ushindani mkali kutoka kwa Snapchat.
Facebook wamesema utafiti unaonesha
wazazi wako radhi kuwaruhusu watoto wao wa miaka 6 hadi 12 watumie mitandao ya
kijamii, mradi wawe wanaweza kufuatilia watoto wao wanafanya nini.
Facebook imeongeza uwezo wa kuhariri
picha na video kuzifanya ziwavutie watoto haki miliki ya Facebook imeongeza
uwezo wa kuhariri picha na video kuzifanya ziwavutie watoto.
Facebook Messenger Kids itahitaji
wazazi kuwafungulia watoto wao akaunti na pia ndio watakaoidhinisha ni watoto
gani wanaweza kuwa marafiki wa watoto wao.
Akaunti ya mtoto inaweza kusimamia
na mzazi kwa kutumia akaunti yake ya Facebook.
Watoto wataruhusiwa kuwasiliana kwa
video, kutuma picha, video na arafa kwa marafiki zao ambao wameidhinishwa na
wazazi wao.
Kwa sasa, mtandao huo wa kijamii
utapatikana Marekani pekee na kwa watu wanaotumia iOS au simu na mitambo ya
Apple.
No comments:
Post a Comment