HABARI PICHA
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza ( wa pili kushoto)
pamoja na Madaktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto wa JKCI na Taasisi ya
Little Hearts ya nchini Saudi Arabia. Mhe. Balozi Mgaza alitembelea Taasisi
hiyo leo kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya kambi ya upasuaji wa Moyo kwa watoto
na watu wazima inayotarajia kuanza siku ya jumapili tarehe 10/12/2017.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi
Mgaza (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari bingwa wa Magonjwa
ya Moyo kwa watoto Naiz Majani na Ali Al-Akhfash wa Taasisi ya Little Hearts ya
nchini Saudi Arabia mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea JKCI kwa
ajili ya kuangalia maandalizi ya kambi ya upasuaji wa Moyo kwa watoto na watu
wazima inayotarajia kuanza siku ya jumapili tarehe 10/12/2017. Jumla ya
wagonjwa 80 wanatarajia kufanyiwa upasuaji wa kufungua na bila kufungua kifua
katika kambi hiyo.
Picha na JKCI
NA MWANDISHI WETU,
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Little Hearts ambao wanafadhiliwa na
Taasisi ya Al- Murtada ya nchini Saudi Arabia wanatarajia kufanya matibabu ya
moyo kwa wagonjwa 80 katika kambi maalum inayotarajia kuanza tarehe 10 –
14/12/2017.
Matibabu yatakayofanyika katika
kambi hiyo ni ya upasuaji wa kufungua kifua na upasuaji wa bila kufungua kifua
(Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab kwa watoto na watu
wazima.
Leo tarehe 08/12/2017 madaktari
bingwa wa Moyo wameanza kufanya uchunguzi kwa wagonjwa wote watakaofanyiwa
upasuaji. Katika kambi hii ya siku tano tumepanga kufanya upasuaji
wa moyo kwa wagonjwa 30 na upasuaji wa bila kufungua kifua kwa wagonjwa 50.
Upasuaji wa kufungua kifua utafanyika zaidi kwa watoto na watu wazima
watafanyiwa zaidi upasuaji wa bila kufungua kifua.
Kwa nama ya kipekee tunaishukuru
sana Serikali kupitia Balozi wetu wa nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza kwa
kutoa kibali cha kuingia nchini (Visa) bila malipo kwa wataalamu wetu hawa
ambao wamekuja nchini kutoa matibabu ya moyo bure kwa wagonjwa wetu.
Kama mnavyofahamu matibabu ya moyo
ni ya gharama hivyo basi tunaendelea kuwahimiza wananchi kujiunga na
mfuko wa taifa wa bima ya afya ambao utawasaidia kulipa gharama za matibabu
pindi watakapougua na kuhitaji kupata matibabu.
metolewa
na:
Kitengo
cha Uhusiano na Masoko
Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete
08/12/2017
|
No comments:
Post a Comment