![](https://www.eatv.tv/sites/default/files/inline/images/KWASI%20LIPULI.jpg)
NA ISSA RAMADHANI.
KLABU ya soka
ya Lipuli FC hapa nchini imesema mlinzi wao Asante Kwasi (PICHANI) ,bado ni mchezaji wao halalia katia kikosi hicho na
alitakiwa kuripoti kambini tangu Disemba 16 mwaka huu lakini hajafanya katika hivyo
hadi sasa.
“Asante Kwasi tulimpa ruhusa ya kuhudhuria msiba wa baba yake nyumbani kwao Gahan na alitakiwa kurudi Disemba 16 na tulifuata taratibu zote ikiwemo kumtumia pesa ya tiketi ya ndege pamoja na mshahara wa mwezi uliopita lakini hadi sasa hajafika hivyo tunashindwa kuelewa”, amesema Sanga.
Siku za hivi karibuni haswa wakati huu wa dirisha dogo la usajili kumekuwepo na taarifa mbalimbali, kuwa mlinzi huyo ambaye amefunga mabao matano hadi sasa kwenye ligi kuu, amesajiliwa na klabu ya Simba japo vinara wa ligi hiyo hawajatoa taarifa juu ya usajili wao.
Hata hivyo tayari Lipuli imeshaweka hadharani majina ya wachezaji walioachwa na waliosajiliwa kwenye dirisha dogo. Kwa walioachwa ni Waziri Ramadhani, Mussa Ngunda, Machaku Salum, Melvin Alistoto, Dotto Kayombo na Ahmeid Manzi.
Kwa waliosajiliwa ni Jamal Mnyate kwa mkopo kutoka Simba, Adam Salamba kutoka Stand United, Alex Ntiri kutoka Mbao FC ambaye ni raia wa Ghana, Miraji Mwilenga na Awadi Mauya kutoka Mufindi United pamoja na Steven Mganga kutoka Pamba FC
No comments:
Post a Comment