Rais
wa Afrika Kusini na mkuu wa chama cha ANC Jacob Zuma
|
SOUTH
AFRICA,Cape Town
CHAMA tawala nchini Afrika Kusini ANC kinaanza mkutano
wa siku tano kuanzia juzi Jumamosi kuchagua kiongozi mpya kika mchuano mkali wa
pande mbili ambao unaonekana kama wakati muhimu katika historia ya taifa hilo baada
ya ubaguzi wa rangi.
Mshindi atakaye
patikana ataandaliwa kuwa rais ajaye wa nchi hiyo , lakini chama cha ANC
kimepoteza umaarufu wake kwa kiasi kikubwa tangu hayati Nelson Mandela
alipokiweka madarakani katika uchaguzi wa mwaka wa 1994 ambao uliweka ukomo wa
utawala wa wazungu wachache.
Rais Jacob Zuma
ambaye utawala wake umakumbwa na kashfa za rushwa , atang'atuka madarakani kama
kiongozi mkuu wa ANC lakini atasalia kuwa mkuu wa nchi kuelekea uchaguzi mkuu
mwaka 2019.
Kuongezeka kwa
ukosefu wa ajira na serikali ya rushwa vimechangia kuchanganyikiwa miongoni mwa
mamilioni ya watu maskini wa Afrika Kusini ambao wanakabiliwa na makao duni na
elimu pamoja na kuendelea kwa ubaguzi wa rangi.
Wanaowania uongozi
wa chama ni mke wa zamani wa rais Zuma, aliyekuwa mkuu wa Umoja wa Afrika
Nkosazana Dlamini-Zuma, na Naibu Rais Cyril Ramaphosa, mfanyabiashara tajiri.
Mpambano huo
unaweza kukigawa chama cha ANC na mkutano huu wa siku tano unatishia kuwa
mbaya, na kulazimisha wagombea wote kutoa wito wa mwisho kuhusu umoja.
No comments:
Post a Comment