Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa
kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni
98 leo jijini Dar es salaam
NA MWANDISHI
WETU
WAZIRI
Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
amewaelekeza Waganga Wakuu wa Mikoa wote nchini kuanzisha zoezi la wazi la
uchunguzi wa saratani ya kizazi angalau mara moja katika mwezi ili kusaidia
kutokomeza tatizo kwa wanawake hilo nchini.
Hayo
yamesemwa leo wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya
shilingi milioni 98 ambavyo vimetolewa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya
JHPIEGO kwa kushirikiana na USAID ili kusaidia kupambana na tatizo hilo nchini.
“Angalau ifikapo Desemba 2018 nataka vituo vya
Afya vya Serikali 524 viwe vinatoa huduma ya matibabu ya awali ya
Saratani ya mlango wa kizazi na kufikia wanawake milioni 3 watakaopata
huduma hii ili kuokoa wanawake wa vijijini kwani mpaka sasa hivi tunavyo
vituo vya afya 265 vinavyotoa huduma hii ” alisema Waziri Ummy.
Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akipokea moja ya vifaa vya uchunguzi wa saratani
ya kizazi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia
Zoungran kushoto wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kuchunguza saratani ya
kizazi leo jijini Dar es salaam.
Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akipokea moja ya vifaa vya uchunguzi wa saratani
ya kizazi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia
Zoungran kushoto wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kuchunguza saratani ya
kizazi leo jijini Dar es salaam.
Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya
watendaji wa Wizara ya afya,Jhpiego na USAID wakati wa kupokea vifaa vya
kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98 leo jijini Dar es
salaam, wa tatu kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw.
Jeremia Zoungran na aliyevaa nguo ya pundamilia ni Afisa Afya kutoka USAID Bi.
Ananth Thambinygan .
Aidha
Waziri Ummy amesema kuwa uchunguzi na kutoa chanjo ya Saratani ya mlango wa
kikazi kwa wasichana kuanzia miaka 9 mpaka 14 ili kuweza kupunguza vifo
vitokanavyo na tatizo hilo kwani katika kila wanawake 100 vifo vinavyotokana na
ugonjwa huo ni 32.
Mbali
na hayo Waziri Ummy amesema kuwa katika kuongeza jitihada za kupambana na
ugonjwa huo Serikali imeongeza vituo vya afya 100 kutoka 343 hadi kufikia
443 mwaka huu ili kutokomeza tatizo hilo nchini.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran
amesema kuwa walianzisha mpango wa kupambana na tatizo hilo na kufanikiwa
kuwafikia wanawake elfu 75 kwa mikoa 4 tangu mwaka 2009.
“Mbali
na mikoa hiyo 4 bado tunalengo la kuongeza mikoa mingine 7 ili kuweza kutoa
huduma hiyo kwa ajili ya kuunga mkono Juhudi za Serikali katika kupambana na
Saratani ya mlango wa kizazi ili kuweza kuokoa wanawake wengi zaidi nchini”
alisema Bw. Zoungran.




No comments:
Post a Comment