Vikombe 3 vya kahawa kwa siku 'vinaweza kuwa na faida za kiafya' - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, 24 November 2017

Vikombe 3 vya kahawa kwa siku 'vinaweza kuwa na faida za kiafya'


Kikombe cha Kahawa
Athari za kahawa zinaweza kuwa tofauti kwa kila mtu  


UNYWAJI  wa kahawa kiasi ni salama , na vikombe vitatu kwa siku vya kahawa vinaweza kuwa na faida kadhaa za kiafya , kulinga na utafiti uliofanywa na BMJ.

Utafiti huo ulibaini kuwa unywaji wa kiasi hicho cha kahawa unaweza kumfanya mnywaji kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya ini na saratani na kupunguza kiwango cha klupata kiharus - lakini watafiti hao wanasema hawawezi kuthibitisha kuwa kahawa ndio sababu ya upungufu wa athari hizo .

Unywaji wa kiwango kikubwa cha kahawa wakati wa ujauzito uhaweza kuwa hata hatari , umethibitisha utafiti huo.

Wataalam wanasema hata hivyo kuwa watu hawapaswi kuanza kunywa kahawa kwa sababu za kiafya ama kama njia ya kuzuwia magonjwa.
vikombe vya kahawa

                               Kila kitu kwa kiasi, ukiwemo unywaji wa kahawa

Watafiti katika Chuo Kikuu cha Southampton walikusanya taarifa kuhusu athari za unywaji wa kahawa kwa binadamu kwa mwili wa binadamu kwa ujumla , wakizingatia tafiti zaidi ya 200 , ambazo nyingi kati yake zilikuwa za uchunguza.

Watafiti walipolinganisha watu wasio kunywa kahawa , na wale wanaokunywa takriban vikombe vitatu vya kahawa kwa siku walionekana kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi.

Faida kubwa ya unywaji wa kahawa zilionekana katika kupunguza hatari ya ugonjwa wa ini, pamoja na saratani.

Lakini Profesa Paul Roderick, mmoja wa waandishi wa utafiti huo kutoka kitivo cha tiba katika Chuo Kikuu cha Southampton, anasema utafiti huo haukusema ikiwa unywaji wa kiasi fulani wa kawaha ulileta ulikuwa na mabadiliko fulani.

Watu wakinywa kahawa na kitafunio vya aina ya croissants
Ni vizuri unapokunywa kahawa kuepuka kula vitafunio vyenye sukari
"Masuala kama vile umri,ikiwa watu walikuwa ni wavutaji wa sigara au hapana na ikiwa walifanya mazoezi ya kimwili kwa kiasi fulani pia yalichangia katika athari za unywaji kahawa ," alisema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot