Hatua ya Rita Ora ya kutunza mayai ya uzazi katika miaka 20 yasifiwa na madaktari - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, 24 November 2017

Hatua ya Rita Ora ya kutunza mayai ya uzazi katika miaka 20 yasifiwa na madaktari



LONDON,Uingereza

MWANAMUZIKI  Rita Ora  amefichua kuwa aliweka mayai yake ya uzazi kwenye barafu baada ya miaka 20 alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha Televisheni ya Australia .

Muimbaji huyo ambaye  raia wa Uingereza, ambaye sasa ana umri wa miaka 26 alisemakuwa  madaktari walimfanyia upasuaji wa kuyaondoa mayai hayo mwilini mwake kwasababu " amekuwa akitaka kuwa na familia kubwa".
"Daktari alisema: 'una afya nzuri sasa na itakuwa vema, kwa nini usiyaondoe mayai yako ya uzazi uyatunze , halafu hautakuwa na hofu ya kuwakosa watoto tena ?'," alisema Rita.

Daktari Helen O'Neill, wa chuo kikuu cha London ,anasema: : " Ni bora kuondoa mwilini mwako na kuyatunza mayai yako ya uzazi mapema kuliko kusubiri."
Lakini ni ''hakikisho kamili'' la kupata ujauzuito na wasichana wengi hawawezi kugaramia garama ya upasuaji na utanzaji wa mayai ya uzazi ambayo ni Euro -£5,000 kila mzunguko mmoja wa hedhi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot