NA ODRIAN NICOLAUS
VIJANA wametakiwa kuwa makini na matumizi ya fedha ndogo
ndogo ambazo wengi wao huamini kwamba haziwezi kuwasaidia kwa chochote zaidi ya
kuzitumia katika kununulia vitu vidogo vidogo ambavyo havina ulazima na
kujikuta wakilalamika maisha magumu kila siku.ile hali inaweza
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa kikundi cha Family Frend
(SACCOS) alipokuwa akizungumza na gazeti hili hivi karibuni.ambae pia ni
mwanafunzi wa chuo cha Uuguzi Masana kilichopo jijini Dar es salaam.Boniface
Sangia alisema ‘’hela ambayo unaiyona ni ndogo inaweza ikakufanya siku moja
kijana ukaweza kujiajiri bila kumtegemea mtu yeyote na katika kufanikisha hilo
ni muhimu kwa kijana yoyote kuhahakisha unajiunga katika vikundi hivi vya
kuweka na kukopa fedha’’.
Boniface aliendelea kusema kwamba umoja ni nguvu hivyo mtu
anapojiunga katika vikundi hivi vya fedha mtu unaweza kuweka fedha zako mahali
sahihi na nidhamu ya matumizi inakuwepo kwani mtu un akuwa tayari ushajizatiti
ili ufikie malengo.ukizingatia upo kwenye kikundi ambacho kinazingatia kanuni
na sheria zote za nchi.
‘’Vijana hutumia fedha zao ndogo ndogo katika kununulia
vifurushi vya intanet (bandle),na hutumia muda wao mwingi katika kuperuzi
mitandao ya kijamii tena mambo ambayo hayana faida kwake wakati mtu unaweza
ukajiunga na kikundi au ukaanzisha kikundi ambacho kitakuwezesha kuwekeza hela
ndogo na baadae ukafikia malengo ya kuwa na maisha mazuri’’alisema Boniface.
Naye Mshauri mkuu wa kikundi hicho Charles Kavishe,ambaye
pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St Joseph kilichopo jijini Dar es
salaam,alisema ‘’kwa kweli mimi binafsi tangu nijiunge kwenye hichi
kikundi naamini nitayafikia malengo yangu bila tatizo kwani kupitia hapa
nimejua mengi na hata fedha ndogo nilizokuwa nikifanyia mambo yasiyokuwa na
tija nimeziwekeza na naamini siku moja zitanifikisha kwenye malengo yangu.
Vijana tuache kusema kwamba hakuna kazi au ajira hakuna hasa
kwa wale tulioko vyuoni tunasoma tukiwa na tumaini kubwa la kuajiriwa wakati
unawezaq ukaanza kujitengenezea ajira yako tangu ukiwa chuoni ukiwekeza kwernye
zile fedha ndogo ambazo ni rahisi kuzipata lakini matumizi yake wengi
hatuyajui.alisema Charles.
Vile vile serikali inatakiwa kuwa karibu na vijana
ambao wanajiunga katika vikundi hivi vya kuweka na kukopa fedha hasa katika
suala la kusajili na kufungua akaunti ni vitu ambavyo vinakuwa na milolongo
mirefu wakati mwingine inakatisha tama hivyo wajaribu kuweka urahisi ili vijana
wanaoanzisha vikundi vyao wapate wepesi bila kuvunja sheria na kanuni
zilizowekwa na nchi.
No comments:
Post a Comment