FAINALI ya kwanza katika mchezo wa shirikisho Africa imepigwa mjini Lubumbashi ambapo wenyeji Tp Mazembe wakiwa nyumbani waliikaribisha klabu ya Super
Sport kutoka nchini Afrika Kusini.
Ambapo mchezo huo Tp Mazembe waliibuka kidede kwa
ushindi wa bao mbili kwa moja ushindi ambao hauwapi uhakika kushinda kombe hilo
baada ya mchezo wa pili utakaopigwa nchini Afrika Kusini.
Tp Mazembe walipata bao la kwanza dakika ya
18 ya mchezo huo kupitia kwa Adama Troure kabla ya Sipho Mbuli kuwapatia wageni
bao la kusawazisha, dakika ya 68 kwenye mechi hiyo Daniel Nii Adjei aliipatia Mazembe bao la ushindi.
Mnamo Dakika 10 za mwisho za mchezo huo
zilikuwa chungu sana kwa Super Sports kwani Tp Mazembe walihamia katika goli
lao huku muamuzi wa mchezo huo akiwanyima penati baada ya Solomon Asante
kuchezewa rafu katika eneo la box.(18 area)
Mchezo wa marudiano utapigwa siku nane
zijazo ambapo Super Sport watahitaji ushindi wa bao moja tu ili kuwa mabingwa
wapya wa michuano hiyo huku Mazembe wakihitaji sare tu ili kutawazwa kuwa
mabingwa.
No comments:
Post a Comment