Guardiola awapongeza wachezaji wake. - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, 27 November 2017

Guardiola awapongeza wachezaji wake.

MANCHESTER,England

KOCHA  wa Manchester  City Pep Guardiola, amesema timu yake imeonesha ushindani wa ajabu wakati ikihangaika  kusawazisha na kuongeza bao la ushindi kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England jana dhidi ya Huddersfield.

kocha mkuu wa  Manchester City Pep Guardiola

PIA Guardiola amekiri kuwa kama timu inataka kushinda ubingwa lazima iwe tayari 
kuonesha maajabu kama ilivyokuwa jana huku akisisitiza kuwa wachezaji wake wanatakiwa kuzoea hali hiyo.

TIMU hiyo Manchester City ilitoka nyuma kwa bao 1-0 kabla ya kusawazisha kupitia  Sergio Aguero kisha kuongeza bao la ushindi kupitia kwa Raheem Sterling. Baada ya ushindi huo matajiri hao wa jiji la Manchester wamefanikiwa kuendelea kukaa kileleni wakifikisha alama 37 dhidi ya 29 za wapinzani wao Manchester United wanaoshika nafasi ya pili.


Pia vinara hao wa ligi wamefikia rekodi yao ya mwaka 2015 ya kushinda mechi 11 za ligi mfululizo. Man City jana ilipata ushindi kwa mara ya kwanza tangu Aprili 1995 ikitokea nyuma kipindi cha kwanza kisha kushinda kipindi cha pili.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot