LONDON,ENGLAND.
Manchester United inatarajia kuingia sokoni kunasa
saini ya mshambuliaji mmoja.
Ambapo majina yanayotajwa kuwindwa na Man United ni Antoine Griezmann wa
Atletico Madrid na Gareth Bale anayecheza Real Madrid.
Hata hivyo, kocha wa Man United, Jose Mourinho hadi sasa hajui atamsajili
mchezaji gani kati ya Griezmann au Bale .
Washambuliaji wote wanamvutia Mourinho na atalazimika kuchagua mmoja ili kuongeza kasi na kuimalisha katika safu ya ushambuliaji Man United.
Aidha Mourinho ana Romelu Lukaku na Zlatan Ibrahimovic aliyerejea uwanjani
akitokea katika maumivu ya goti yaliyomuweka nje ya uwanja miezi saba.
Mshambuliaji Griezmann na Bale mmoja kati yao anapewa nafasi ya kuvaa uzi wa
Man United katika dirisha la usajili Januari, mwakani endapo mpango huo
utafanikiwa mapema kabla ya majira ya kiangazi.
Hata hivyo Bale amekuwa na maisha magumu Real Madrid baada ya kuandamwa na
majeraha ya mara kwa mara, lakini Griezmann tangu kuanza msimu huu hayuko fiti.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, amefunga mabao mawili katika mechi 10
alizocheza na mwishoni mwa wiki iliyopita alizomewa na mashabiki wa Atletico
Madrid katika mchezo dhidi ya mahasimu wao Real Madrid.
Msimu uliopita Griezmann alicheza kwa kiwango bora na aliwekwa sokoni akiuzwa
Pauni 200 milioni, lakini Man United ilishindwa kumsajili baada ya Atletico
Madrid kufungiwa na Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) kusajili.


No comments:
Post a Comment